Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 9, 2013

Ivo asimulia alivyocheza penalti ya ushindi Kenya


Kipa amba moja wa Kilimanjaro Stars, Ivo Mapunda.
Na Khatimu Naheka
KIPA namba moja wa Kilimanjaro Stars, Ivo Mapunda, amefurahi kuona juhudi zake na wachezaji wenzake zikisaidia kuivusha timu hiyo kutinga nusu fainali katika michuano ya Kombe la Chalenji lakini akasimulia jinsi alivyoweza kuokoa penalti iliyokivusha kikosi hicho.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ivo amesema mara baada ya kumalizika kupigwa kwa penalti nne za awali huku akiwa amefanikiwa kucheza moja ya Khalis Alucho, alilazimika kubadili mfumo wake wa awali kufuatia Daniel Sserunkuma kuwa mzuri katika upigaji wa penalti.
Ivo anayekipiga katika klabu moja na Sserunkuma, amesema alilazimika kukumbuka haraka namna ambavyo Mganda huyo alivyokuwa akipiga penalti zake wakati wakiwa mazoezini katika klabu yao ya Gor Mahia ya Kenya ambapo alikuwa mtulivu golini akifuatilia kila kitu anachokifanya na kujikuta akiicheza, jambo ambalo lilimfanya afurahi zaidi.
“Kama uliangalia kwa makini baada ya kumalizika kwa penalti nne za awali, ilinibidi niwe mbunifu kwa kubadili namna ambavyo nataka kucheza penalti lakini nilipomuona Danny (Sserunkuma), nilikuwa mtulivu kwa kuwa anajua sana kupiga penalti,” alisema Ivo.
“Nilifurahi sana kuiokoa penalti yake hasa kwa kuwa nimecheza penalti ambayo mpigaji alikuwa hodari sana katika upigaji.”




No comments:

Post a Comment