Wakati hayo yakijiri itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kusherehekea
uhuru wake huku bendera yake ikipepea nusu mlingoti kufuatia msiba
mkubwa uliotokea wa kiongozi mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20
na 21 kiongozi wa kwanza mweusi nchini Afrika ya Kusini Nelson Mandela
aliyefariki dunia mnamo tarehe 5 Desemba 2013 baada ya kuugua kwa muda
mrefu.
Kwa mujibu wa hotuba ya salamu za rambirambi aliyoitoa Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa taifa la watu wa Afrika ya Kusini na
Dunia, Jk alitangaza siku 3 za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8
Desemba 2013 na kuagiza bendera zote kupepea nusu mlingoti.
Na sasa inatajwa kuwa siku moja zaidi imeongezwa (yaani leo tarehe 9
Desemba 2013) kwa ajili ya kuthamini mchango wa Mwamba huo wa Afrika
ulio dondoka
No comments:
Post a Comment