Wageni waalikwa kwenye Red Carpet.
Mtangazaji
wa Televisheni ya Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akiwa kwenye Red Carpet
kabla ya mahojiano na Mkurugeni wa Kajunason Blog Cathbert Angelo.
Afisa
Mtendaji Mkuu na Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji alikuwa ni
miongoni mwa wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Azam TV. Pichani
akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi Mwambulambo.
Mtangazaji
wa Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akifanya mahojiano na Mdau William
Malecela a.k.a LEMUTUZ na Mmiliki wa Blog ya Wananchi.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB)
akizungumza kwenye uzinduzi wa Azam TV uliofanyika Hyatt Regency The
Kilimanjaro Hotel mwishoni mwa Juma ambapo amesema Azam TV imekujali
kuleta mapinduzi katika ulimwengu wa Digitali na kutoa fursa ya ajira
kwa Vijana wa Tanzania wenye vipaji sanjari na kuitangaza nchi yetu
katika bara la Afrika hasa kwenye upande wa Soka na Filamu.
Azam
TV itaanza kurusha matangazo yake Desemba 6 mwaka huu, Watanzania kaeni
mkao wa kula kupata King’amuzi kwa bei rahisi ambacho kitakuwa na
chaneli zisizopungua 50.
Fashi fashi zikipamba uzinduzi rasmi wa Azam TV.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Azam TV kitengo cha Huduma kwa Wateja wakiwa
wameshikilia Ving’amuzi vya Azam TV wakati wa uzinduzi huo.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January
Makamba (MB) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Azam TV mara
baada ya kuzindua rasmi kwenye sherehe zilizofanyika mwishoni mwa Juma
Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba (MB)
katika tete-a-tete na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd. Rhys
Torrington mara baada ya kuzindua Azam TV itakayoanza kurusha matangazo
yake hewani Desemba 6 mwaka huu.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Azam Tv, Rhys Torrington akizungumza na wageni
waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Azam Television jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa Juma.
Mkurugenzi wa vipindi wa Azam Tv Efe Atiyio akifafanua juu ya program mbalimbali za Azam Tv .Na MO BLOG
Yusuf Bakhresa akizungumza jambo na watoto wake kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Concepts Limited, Benny Kisaka (katikati) alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa uzinduzi huo.
Yusuf Bakhresa akibadilishana mawazo na wadau wa michezo nchini waliohudhuria uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Aggrey & Clifford Bw. Rashid Tenga naye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Bw. Boniface Wambura (kushoto) akifuatilia yanayojiri kwenye uzinduzi huo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mh Mohammed Dewji (MB) akifurahi jambo na wadau.
Mtangazaji
maarufu wa Radio One na ITV Maulid Kitenge na Mfanyabiashara maarufu
CEO wa Delina Group Enterprises Bw. Davis Mosha wakifurahi jambo wakati
wa uzinduzi huo.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa makampuni ya SSB Ltd. Said Muhammad Said (wa pili kushoto)
akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za
Bakhresa.
Mdau Omar Said ( wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake kwenye picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment