Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)
Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari (Hawapo pichani)
bunduki aina ya shortgun iliyokutwa nyumbani kwa mtu anayejulikana kwa
jina na Jumanne Abdallah Maarufu kwa jina la Babu G (25) Unga Ltd jijini
hapa ambaye anatuhumiwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya ujambazi
hapa nchini. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)
Liberatus Sabas akionyesha risasi zilizokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa wa
ujambazi Jumanne Abdallah maarufu kwa jina la Babu G maeneo ya Unga Ltd
jijini hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Mtu
mmoja anayetuhumiwa kwa ujambazi ajulikanaye kwa jina la Jumanne
Abdallah Maarufu kwa jina la Babu G (25) Mkazi wa Unga Limited jijini
hapa amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa na bunduki aina ya short gun
pamoja na risasi 13 zinazotumika katika bunduki ya aina hiyo.
Bunduki
hiyo yenye namba C. 056900 iliyokuwa imekatwa kitako na mtu ilikutwa
nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, maeneo ya Unga Limited katika Halmashauri
ya jiji la Arusha mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa kutoka
kwa raia wema.
“Mara
baada ya kupata taarifa, askari wetu walikwenda katika nyumba hiyo muda
wa saa 2:30 asubuhi na kumkuta mtuhumiwa katika chumba chake ambaye kwa
wakati huo alikuwa anajiandaa kutoka, ndipo walipomkamata kisha kufanya
upekuzi katika chumba hicho na kuikuta silaha hiyo pamoja na risasi
hizo”. Alisema Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas.
Kamanda
Sabas aliendelea kusema kwamba, mara baada ya mtuhumiwa huyo kuhojiwa
na Jeshi la Polisi mkoani hapa, alikiri kuhusika katika matukio
mbalimbali ya uhalifu kama vile unyang’anyi wa kutumia nguvu na silaha
katika maeneo mbalimbali hapa nchini huku akiwataja wenzake ambao
wanaendelea kutafutwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani pindi
upelelezi utakapokamilika.
Kamanda Sabas ameendelea kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment