Hali hii ni tofauti kwa Oliver Matemu, ambaye juhudi zake zimebadilisha maisha yake ndani ya miaka 15.
Matemu
ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kipipa Millers Limited, ambayo hivi
karibuni iliibuka kinara kwenye shindano la kuzisaka kampuni ambazo
zinazokua kwa kasi nchini.
Shindano
hilo la Kampuni 100 (Top 100 Mid–Sized Companies), linaendeshwa na
Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) na KPMG Tanzania, na
kudhaminiwa na Benki ya NBC pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam
(DSE).
Matemu
anasema alianza biashara yake mwaka 1998 akiwa mkoani Mbeya na alikuwa
akinunua unga wa mahindi kwenye mashine za watu na kusambaza kwenye
maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na shule. “Biashara yetu tulianza na
mtaji wa Sh1.5 milioni na nilikuwa nikinunua unga na kuuza kwenye
taasisi kama shule, wakati mwingine tulikuwa tunasambaza pamoja na
mchele.
Ilipofika
mwaka 2005 nilichukua mkopo nikanunua mashine za kusaga na kukobua
nafaka, pale Mbeya nilipoamia Mwanza nikahama na mashine zangu,” Anasema
Matemu. Anasema kwa mwaka sasa anafanya biashara ya wastani wa Sh5
bilioni kutoka mtaji wa Sh1.5.
Nilianza na kilo 20
Mbali ya kusaga na kusambaza nafaka, pia alikuwa anasambaza vinywaji vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Wakati huo mama huyo alikuwa akifanya biashara huku akiwa ni mwalimu wa shule ya sekondari.
“Nilikuwa
nafanya shughuli zangu huku nikiendelea na kazi yangu ya ualimu, kazi
ya ualimu niliifanya kwa miaka 12, baadaye nilipata tatizo la mkono wa
kulia, nikaona siwezi kuendelea kufundisha nikaamua kuongeza nguvu
kwenye biashara zangu,” anaeleza Matemu.
Mfanyabiashara huyo alianza biashara kwa kununua unga kilo 20 na kuusambaza, lakini sasa anasambaza tani 15 za unga kwa siku.
“Hii biashara ya msimu, wakati ukikuta tuna tenda kubwa tunasambaza mpaka tani 15 kwa siku,” anasema.
-MWANANCHI
No comments:
Post a Comment