Mashabiki wa Timu ya Simba, wakimpokea kwa shangwe na nderemo, kocha wao mpya aliyetua nchini jana machana.
Kocha huyo akikabidhiwa taji la maua na mashabiki baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar leo.
Mara
kadhaa kumekuwa kukitokea furaha kwa mashabiki, viongozi na hata
wachezaji wa Klabu zetu kubwa hapa nchini, wakati wanapokuwa
wanamkaribisha Kocha mpya ama kumtambulisha kwa mbwembwe nyingi, lakini
anapotokea kukosea kidogo haijalishi ni muda gani amekwisha kaa na Klabu
husika, anaweza kutimulia ama kuanzishiwa mizengwe hadi akakata tamaa
ya kuonyesha yale yote aliyojiandaa nayo kuifanyia Klabu husika.
Wakati
umefika sasa kwa Klabu zetu kufunguka kifikra na kuwa na upeo wa
kufikiri ili kuziendeleza klabu zetu, kwa kuwaachia makocha waweze
kufanya yale yanayostahili bila kuingiliwa na viongozi ama watu flani
kwa pesa zao ama umaarufu wao katika klabu. Huko nyuma
walikwishapokelewa makocha kadhaa kama alivyofanyiwa kocha huyu leo na
waliondoka kimya kimya huku wengine wakiondoka klabuni kwa mafalakano na
viongozi wa klabu.
Akipata menu.
Kocha
huyo akiongozana na baadhi ya viongozi wa Simba wakati alipotembelea na
kukagua uwanja wa mazoezi wa Klabu hiyo wa Kinesi.Picha kwa Hisani ya
Lenzi ya Michezo
No comments:
Post a Comment