Pages

Saturday, December 7, 2013

Polisi wataja sababu za ongezeko la ukatili wa kijinsia

POLIS_71f55.jpg
Na John Banda, Dodoma
DAWATI la kupinga ukatili wa kijinsia na watoto lililopo katika mpango wa polisi jamii limetangaza jumla ya makosa 2425 yanayohusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kuwandiyo yaliyoripotiwa polisi mkoani Dodoma kati ya Januari 2009 mpaka octoba mwaka huu.

Hayo yalisemwa na mkuu wa Dawati hilo [ASP] Hamida Hiki wakati wa madahalo wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kati.
Alisema makosa ya ukatili wa kipigo yalikuwa 1020, yakifuatiwa na ubakaji 794, shambulio 411, Ulawiti 179 kutupa watoto 14 ma matukio saba ya wizi
wa watoto.

Alizitaja changamoto katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ni jamii bado ina mfumo dume hivyo kuwa chanzo cha ukatili, kuendelea kuwepo kwa mila potofu kama ukeketaji na kuozesha mabinti wakiwa na umri mdogo, kuongezeka kwa wimbi la watoto wa mitaani, ulevi wa kupindukia na matumizi ya madawa ya kulevya.
Pia hali duni ya uchumi inayopelekea kushamiri kwa biashara ya binadamu hasa kwa wasichana kupelekwa mijini kutafuta ajira na mashahidi kushindwa
kujitokeza kwa wakati kwa ajili ya kutoa ushahidi mahakamani.

Alisema tangu kuanzishwa kwa dawati la jinsia miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni ongezeko la kesi za unyanyasaji wa kijinsia kuripotiwa tofauti na awali waathirika walikuwa hawatoi taarifa kwenye vituo vya polisi.
Pia jamii kuwa na imani na Jeshi la Polisi hivyo ushirikiano na mahusiano katika suala la kupinga vitendo vya ukatili umeongezeka, kuboreshwa kwa
huduma za jinsi na kushughulikia makosa ya jinsia na watoto ambapo huduma hizo sasa zipo hadi ngazi ya vituo vidogo.

Nae Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali linalopinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto (AFNET) Sarah Mwaga anaitaka jamii kutoa ushirikiano ili vitendo vinavyohusiana na ukatili wa kijinsia vikomeshwe.
Mdahalo huo uliandaliwa na Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa kijinsia (MKUKI) ulioratibiwa na AFNET kwa kushirikiana na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) Tanzania na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.
Mwisho


TUNAOMBA BOFYAHAPA LIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI NA ZA KUSISIMUAAA(USIPITWEEE)



No comments:

Post a Comment