Katika barua yake hiyo, Rais Kikwete amemtaka Tenga asichoke kutoa ushauri na uzoefu wake kila utakapohitajika katika shughuli mbalimbali zinazohusu maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.
Rais Kikwete alikuwa akiijibu barua ya Tenga iliyokuwa ikimuarifu kuhusu kumaliza kipindi chao cha uongozi na kumshukuru yeye binafsi (Rais Kikwete) na serikali anayoiongoza kwa mchango waliotoa katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
“Pongezi zako zimetupa moyo na ari ya kuongeza maradufu juhudi zetu za kuboresha kiwango cha ubora wa mchezo wa mpira wa miguu nchini.
“Kwa niaba ya serikali, napenda kuchukua nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwako wewe na uongozi wote uliopita wa TFF kwa mchango wenu muhimu mlioutoa wa kuendeleza mpira wa miguu nchini.
“Mafanikio ya kutia moyo yamepatikana chini ya uongozi wako,” alisema Rais Kikwete katika barua yake hiyo na kumtakia kila la heri Tenga katika shughuli zake.
Tenga ambaye hivi sasa ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), aliiongoza TFF kwa vipindi viwili kuanzia Desemba 2004 hadi Oktoba 2013.
No comments:
Post a Comment