Wapenzi
wa movie za The Fast and the Furious watakuwa wanamfahamu Paul Walker
vizuri ambapo ameshiriki kikamilifu kwenye movie za Fast and Furious.
Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao hadi ku-trend kwenye mitandao
mbalimbali ya kijamii ni kuhusu kifo cha muigizaji huyu ambapo taarifa
rasmi zinasema alikuwa anatoka kwenye event ya kujitolea ya organisation
yake inaitwa Reach out World Wide.
Paul Walker akiwa kwenye safari ya kurudi kutoka kwenye hiyo event
ndani gari la kifahari lenye viti viwili aina ya Porsche Carrera GT,
ambapo yeye alikuwa abiria na rafiki yake akiwa dereva wa gari hilo ndio
wakapata ajali.
Habari zinasema kwamba dereva huyo alipoteza control na kuvamia mti au nguzo na gari kuanza kuwaka moto.
Polisi hawajathibisha rasmi chanzo cha ajali hiyo lakini hadi hivi
sasa inasemekana kuwa ni speed kali ambayo ilimfanya dereva ashindwe
ku-control gari hilo.
Paul amefariki akiwa na miaka 40 na ameacha binti mwenye miaka 15
Wadadisi wa mambo ya kibiashara
wameshaiangalia Fast and Furious 7 kwamba itafanya vizuri sokoni
kwasababu hiyo ndio itakuwa movie ya mwisho ya Paul Walker na itatoka
July 11, 2014.
Hii
picha ilipigwa muda mfupi kabla ya ajali kutokea akiwa anaondoka kwenye
event ya kujitolea na hilo ndio gari lenyewe kabla ya ajali
Juu na chini ni baadhi ya scenes Paul Walker alizoshiriki kwenye Fast and Furious
No comments:
Post a Comment