Mkuu
wa kitengo cha utalii cha Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) Bw.
Mombo akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Balozi
Charles Sanga (kushoto) na Meja Jenerali mstaafu Gimonge kuhusu njia
mbalimbali zinazotumika katika kupanda mlima Kilimanjaro muda mfupi
kabla ya Balozi Sanga kuanza kuongoza msafara wa kupanda mlima.Msafara
wa Uhuru expedition katika picha ya pamoja na waongoza wapamda mlima
muda mfupi kabla ya kuanza kupanda mlima Kilimanjaro kupitia njia ya
Marangu.
Mwenyekiti
wa TTB Balozi Sanga (wa pili kushoto)sambamba na wapanda mlima
expedition wakichanja mbuga kuelekea kituo cha Mandara.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania – TTB anaongoza timu
ya watu saba miongoni mwao wakiwemo wafanyakazi wa Bodi ya Utalii
Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro ambao pia ni mrefu kuliko yote barani
Afrika na ambao pia ni miongoni mwa maajabu saba ya asili barani
Afrika.
Msafara huu ujulikanao kama Uhuru Expedition ambao
ni mahsusi kwa ajili ya kuadhimisha miaka 52 ya uhuru umeratibiwa na
kufadhiliwa na Bodi ya Utalii Tanzania umeanza kupanda mlima Kilimanjaro
tarehe 6/12/2013 umeanza kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 6/12/2013
umeanza kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 6/12/2013 kupitia njia ya
Marangu na unatarajia kumaliza zoezi hilo tarehe 10/12/2013.
Msafara
huo wenye jumla ya wapandaji mlima saba (7) ambapo kutoka TTB ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Charles Sanga, Bw. Musa Kopwe
na Bw. Hillary Mushi. Aidha katika msafara huo yumo pia Meja Jenerali
mstaafu Gimonge, Bley Mayo, Bibi Lidya Kayuni na Bw. Joan Mwamlima wote
kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Hii
ni mara ya pili kwa Bodi ya Utalii Tanzania kuratibu msafara huu kwa
lengo la kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania Bara. Mara ya kwanza kwa
TTB kufadhili Uhuru Expedtion ilikuwa ni mwaka jana ambapo pamoja na
TTB Kampuni nyingine kama ya bia ya Serengeti ilijitoleza pia kudhamini
Msafara huo wa Uhuru ulioongozwa na aliyekuwa mkuu wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali mstaafu George Waitara.
No comments:
Post a Comment