Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 2, 2013

TUZO ZA NZUMARI ZA KENYA ZASHINDWA KUFANYIKA

Nzumari za Mombasa, Eve ‘Queen’ Adhiambo amelazimika kuziahirisha tuzo za mwaka huu katika dakika za mwisho kutokana na mahudhurio hafifu na maandalizi ya zimamoto. 540394_3265740004763_16594435_n Eve
Hadi saa nne usiku, sound system na jukwaa vilikuwa havijawekwa na watu wachache waliokuwa wamehudhuria walilazimika kurudi makwao baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya ukumbi sababu mambo yalikuwa hayajakaa sawa. Eve ambaye alionekana kupagawa wazi alisema kuwa watu waliokuwa wameenda
walidanganya na watu wachache getini kwamba show hiyo ilikuwa imeahirishwa.
“Unajua kulikuwa na watu kwenye geti waliokuwa wakiwahadaa watu waliokuwa wamekuja kwa kuwaambia kuwa tukio lilikuwa limeahirishwa, hizi ni tetesi kubwa na nahisi iliwafikia hata wale waliokuwa wamepanga kuja,” Eve aliiambia website ya ommydallah.com. “Ntalazimika sasa kusitisha tukio hili mpaka ntakapotangaza tena kwakuwa bado nahitaji kuwatuza washindi,” aliongeza. Eve aliwalaumu pia wafundi wa sauti aliowapa kazi kuishughulikia na kusema kuwa walichelewa kwenda.Hata hivyo mmoja wa mafundi hao aliiambia tovuti ya . Ommydallah kuwa ni Eve ndiye alichelewa kuwataarifu. “Huyu demu sisi mwanzo alitufuata jana (Friday) akitaka sound then sasa leo ndio akaja vizuri tena saa tisa na sisi mdosi akatutuma kazi na tukaja, lakini nadhani shida ilikuwa ni mambo na pesa maana watu wengi hapa wanaogopa kufanya kazi na huyu dem,” alisema. Eve alikanusha madai hayo na kusema kuwa kilichotokea ni hujuma. “Unajua sipendi kumtukuza shetani na nikisema kuwa kuna mkono wa mtu nitakuwa namtukuza ila ningependa kusema kuwa usishangilie wakati mwenzako amepatakina na shida kama hii maana kesho inaweza kuwa wewe,” alisema. Rapper Nay wa Mitego aliyekuwa ameenda Mombasa kuhudhuria show hiyo alilazimika kulipia mwenyewe gharama za malazi na tiketi ya ndege kurejea Dar kwakuwa mwandaaji hakuweza kuingiza fedha za kuweza kulipa gharama hizo. “Unajua kaka me nimetoka Nairobi kushoot clip na nikaunganisha direct na hapa but mambo ni kama unavyoyaona, cha msingi nilichokua nataka kutoka kwao ni wanipe ticket yangu ya ndege tu ya kurudi bongo asubuhi maana nina show na Diamond kesho,” ameiambia tovuti hiyo. “Kama bahati mimi hutembea na hela zangu mfukoni maana nayajua mambo haya sasa itabidi nijilipie tu kila kitu na hela yangu.” Hata hivyo Nay aliyekuwa ametajwa kuwania tuzo hizo amesema amemsamehe Eve. “Yani kulingana na heshima na ukubwa wangu unadhania mimi nastahili kuhangaika hivi?!! inakera sana ila huyu dada mimi nishamsamehea.” Drama nyingine iliyotokea ni baada ya Eve na timu yake kuamua kuondoka ukumbini ambapo watu waliokuwa wamelipa kiingilio walimfuata kudai warudishiwe chao. Watu hao walirushiana maneno na timu ya Eve japo hawakuambulia chochote. Rich Mavoko alikuwa ahudhurie show hiyo pia lakini machale yalimcheza. Pamoja na Nay Wa Mitego wasanii wengine waliokuwa wametajwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na Ommy Dimpoz, Lady JayDee na Rich Mavoko

No comments:

Post a Comment