.Jaji Manento asema ni uvunjifu wa sheria kwenda na watoto harusini
Na Damas Makangale, MOblog
WAZAZI
na Walezi wameaswa kuacha mara moja tabia ya kwenda na watoto katika
sherehe na harusi mbalimbali za kwa sababu ni kosa la Jinai kwa mujibu
wa sheria na Haki za Mtoto. MOblog inaripoti.
Akizungumza
kwenye mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ambao
huadhimisha kila tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka, Mwenyekiti wa Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, Jaji Mstaafu Amir
Manento amesema kwa mujibu wa sheria na Haki za Mtoto wazazi au walezi
hawaruhusi kwenda na watoto katika sherehe za usiku.
“wazazi
na walezi na watu wa kawaida wanamazoea ya kwenda na watoto kwenye
sherehe za harusi na majumba ya starehe lakini kwa mujibu wa sheria na
haki za mtoto na marekebisho yake ya 2009 ni uvunjifu wa sheria na haki
za mtoto,” amesema Jaji Manento.
Amesema
kuwa Tanzania iliridhia tamko rasmi la Haki za Binadamu ili pamoja na
mambo mengine kulinda Uhuru na Haki za Binadamu pamoja na haki ya
kuishi.
“Tarehe
10 Disemba imeainishwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.
Kuainishwa siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu kunakumbusha juhudi
kubwa zilizofanywa kwa lengo la kuwafanya watu waheshimu Haki za
Binadamu kote duniani,” alisisitiza.
Jaji
Manento amesema suala la kuheshimiwa haki za binadamu lilipewa
kipaumbele cha kwanza wakati wawakilishi wa nchi mbalimbali walipokuwa
wakibuni Hati ya Umoja wa Mataifa.
Aliongeza
kuwa Januari mwaka 1947 iliundwa kamati ya haki za binadamu na hati ya
kamisheni hiyo ilipasishwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe
10 Disemba 1948.
Jaji
manento amesema kuwa kwa msingi huo siku hiyo ya tarehe 10 Disemba
ilitambuliwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu duniani kote.
Amesema
kuwa imepita zaidi ya miongo sita sasa tangu kutolewa Azimio la Haki za
Binadamu ambalo linakusanya thamani za pamoja kwa ajili ya kuondoa
ubaguzi, kueneza uhuru na kupambana na dhuluma dhidi ya binadamu
duniani.
Alilisitiza
kwamba hapana shaka kuwa kutetea haki za binadamu kwa ajili ya kutimiza
lengo hilo ni kazi yenye thamani kubwa. Hata hivyo aliongeza kadhia
hiyo inayumbishwa na nchi za Magharibi ambazo zinatumia haki za binadamu
na ripoti zinazotolewa na taasisi za haki za binadamu kama nyenzo na
fimbo ya kisiasa kwa baadhi ya nchi zinazoendelea.
Kauli
mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ni “mafanikio na
changamoto katika kuhamasisha na kulinda Haki za Binadamu Tanzania” .
No comments:
Post a Comment