Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 2, 2013

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA ATEMBELEA OFISI ZA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO


Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makame Mbarawa( Kushoto) pamoja na msafara wa Waziri Mkuu wakielekea katika kituo maalumu cha uangalizi wa mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura kuhusu baadhi ya mitambo iliyopo nje ya jengo la Simu (Telephone House). Wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makame Mbarawa.
Afisa Mtendaji wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akitoa taarifa fupi kuhusu utendaji wa TTCL na jinsi kamuni hiyo ilivyojidhatiti katika kujenga, kusimamia na kuendesha mkongo wa Taifa wa Mawasilino.
Afisa Mtendaji wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akimuonesha waziri mkuu mkongo halisi (fibre) wakati wa ziara yake katika kituo maalum cha uangalizi wa mkongo wa Taifa (Network Observation Centre).
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akipata maelezo namna mitambo ya mkongo wa taifa inavyofanya kazi kutoka kwa Mhandisi Adam Mwaipungu wakati wa ziara yake katika ofisi hizo.

No comments:

Post a Comment