Pages

Tuesday, January 21, 2014

ALIYEKUA KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA SASA MKOA WA TANGA NDUGU SALUM MOHAMMED CHIMA AAGA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA TAYARI KWENDA KURIPOTI TANGA

Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Tanga aliyehamishwa kutoka Mkoa wa Rukwa Ndugu Salum Mohammed Chima akizungumza katika hafla fupi ya kuagana na uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya (kulia) leo baada ya mabadiliko ya hivi karibuni ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete ambapo ameteua Makatibu Tawala wapya watano na kuhamisha wengine akiwepo Ndugu Salum Chima. Katika salamu zake za kuaga ameomba viongozi wote wa Mkoa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanasimamia kikamilifu na kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa ya Serikali na wahisani mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa salam zake za maagano ambapo alisikitika kwa uhamisho wa kiongozi huyo ambaye kwake alikua kiungo muhimu na msaada mkubwa katika mambo ya kiutendaji. Aidha alisisitiza juu ya kuchapa kazi na ushirikiano baina ya viongozi wa Mkoa na wananchi katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akitoa neno kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Rukwa, alisema kuwa kwa Ndugu Chima kuhamishiwa Mkoa wa Tanga ambao ni Jiji akitokea Mkoa mdogo wa Rukwa ni “promotion” na anastahiki pongezi kwani uwezo wake wa kuchapa kazi ndo umemfikisha hapo alipo. Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa sifa kubwa ya Ndugu Chima ni uwezo wake mkubwa wa kutoa maamuzi sahihi na ya haraka kwa wakati sifa ambayo ni muhimu kwa viongozi wa sasa katika maendeleo ya taifa letu.
Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Ndugu Samson Mashalla (kulia) akiongea kwa niaba ya watumishi wote wa Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa. Alieleza kushtushwa na uhamisho huo uliokuwa wa ghafla ambapo kwa watumishi umekuwa ni kusikitisha kutokana na ukaribu, upole na upendo aliokuwa nao Ndugu Chima. Ndugu Chima aliwapenda watumishi wote wa ngazi za juu hadi za chini bila ubaguzi wa aina yeyote.
Baadhi ya viongozi na watumishi walihudhuria katika hafla hiyo fupi ya maagano. WATUMISHI WOTE NA VIONGOZI WA SERIKALI YA MKOA WA RUKWA WANAMTAKIA NDUGU CHIMA KILA LA HERI KATIKA KITUO CHAKE KIPYA CHA KAZI AMBACHO NI MKOA WA TANGA. Tunaamini kuwa Tanga imepata kiongozi thabiti mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza katika kutoa maamuzi sahihi na ya haraka kwa muda muafaka, “tunaomba apewe ushirikiano atafanya”. Kwa upande wake Katibu Tawala Mteule wa Mkoa wa Rukwa kwa sasa ndugu Symthies E.Pangisa aliyekuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara anakaribishwa kwa dhati Mkoani Rukwa na ameahidiwa ushirikiano katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. 
(Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment