Pages

Wednesday, January 29, 2014

CCM WASHANGAA HELIKOPTA YA CHADEMA

nchembaNa Mwandishi wetu, Arusha
Chama cha mapinduzi (CCM)kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha
chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)kutumia Helikpota kwenye
chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni
kujitafutia sifa na umaarufu pekee  kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu mkuu wa CCM ambaye pia ni Naibu waziri
wa fedha Mwigulu Nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za  udiwani

katika kata ya Sombetini .
Mwigulu alisema kuwa CCM inashangaa sana Chadema kutumia Helikpota
kwenye chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo wanaonesha wazi kuwa
wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa kwani gharama
ambazo zinatumika hadi kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya Milioni 200.
Alisema kuwa Gharama ambayo inatumika kwenye uendeshaji wa Helkopta ni
gharama ambayo ingeweza kuwasaidia wanachama  wao lakini hata matumizi
mbalimbali ya chama hicho ambacho bado kinaonekana kukabiliwa na
changamoto nyingi sana

“wananchi wa kata ya Sombetini napendwa kuwaambia kuwa hata sisi
wenyewe huwa tunashangaa sana ujio wa hii Helikopta na ninapenda
kusema wazi helikopta hiyo inakuja ili iweze kuwazubaisha ninyi sasa
msikubali kudanganywa na helikopta baliangalieni sera za mgombea
“aliongeza Mwigulu
Pia aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa kamwe hawatumiki kwenye siasa
za sifa na ushahbiki kwani siasa hizo wakati mwingine zinasababisha
hata vifo vya watu ambao hawana hatia ya kufa ovyo
“wananchi mnapswa kujua na kutambua kuwa siasa za sasa zimebadilika
sana msikubali kuwa mashabiki wa siasa bali mnatakiwa kuangalia zaidi
sera za vyama na mahitaji yenu msije mkachagua kiongozi kwa ushabiki
itawagharimu sana kwenye utendaji”aliongeza Mwigulu
Awali Mgombea Udiwani katika kata hiyo ya Sombetini kwa tiketi ya CCM
alisema Bw David Mollel alisema kuwa ana mikakati mingi sana ya
kuhakikisha kuwa anasaidia kata hiyo endapo kama atapata ridhaa ya
kuongoza rasmi kama diwani
David alisema kuwa changamoto ambazo atahakikisha kuwa ameweza
kuzitatua ni pamoja na urekebishaji wa barabara, uboreshaji wa masoko,
kna uimarishaji wa vikundi vya wanawake na jamii kwa ujumla

No comments:

Post a Comment