Mmoja wa wanachama watatu wa CHADEMA waliovuliwa nafasi zao za uongozi ndani ya chama, Zitto Kabwe kupitia kwa Wakili wake, Alberto Msando, leo ameanza kufanya ‘FORUM SHOPPING’ kwa kupeleka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania, akiomba Kamati Kuu isijadili na kuamua jambo lolote kuhusu uanachama wake, kwenye kikao maalum kinachofanyika leo.
Awali
muombaji kwa namna ambayo inaweza kuitwa kuwa ni kuvizia, alitaka
Mahakama Kuu hiyo itoe amri kutokana na ombi lake hilo, bila upande wa
chama kuwepo mahakamani, lakini kwa bahati nzuri mawakili wa chama,
Mwanasheria Mkuu wa chama, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Sheria na Haki
za Binadamu, Peter Kibatala; wakafanikiwa kuwepo kortini, hivyo
wakawa-served maombi hayo kisha mahakama ikalazimika kusikiliza
Preliminary Objections (PO) kutoka kwa mawakili wa CHADEMA dhidi ya
waleta maombi.
Maombi
hayo ya wakili Msando kwa niaba ya Zitto yamefunguliwa mahakamani dhidi
ya Baraza la Wadhamini CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama.
Hoja
za mawakili wa CHADEMA katika PO zilikuwa ni katika maeneo matatu
ambayo ni vifungu vya kisheria ambavyo waombaji walikosea;
1.
Vifungu vya sheria walivyotumia waombaji kuomba court injunction,
haviipatii Mahakama Kuu mamlaka ya kufanya maamuzi hayo wanayoomba
ifanye. Kwa sababu kwa ujumla ukikosea vifungu hasa vinavyohusu msingi
wa kesi, ni sawa na kwamba hakuna kesi.
2. Hati ya kiapo ya waleta maombi haikuwa na facts kama inavyotakiwa badala yake ilikuwa imejaa maneno ya ubishi ubishi.
3.
Mahakama haiwezi ku-entertain kusikiliza migogoro ya ndani katika vyama
vya hiari mf; vyama vya siasa, dini na michezo (ambavyo uanachama wake
ni wa hiari), kwa sababu mojawapo ya principle ni kwamba ili mtu awe
mwanachama anakuwa amekubaliana na katiba, kanuni, taratibu na makatazo
ya chama husika.
Aidha
katika maombi yake kuna vitu vingine ‘muhimu’ ambavyo mleta maombi
amejikuta akivionesha kuwa anakubaliana na taratibu za chama lakini
wakati huo huo tena anataka mahakama imsikilize;
· Amekiri kuwa amevuliwa nafasi za uongozi na amekata rufaa
· Amekiri kuwa ameandikiwa mashtaka kwa maandishi na yeye amejibu
· Amekiri kuwa ameandikiwa kuitwa mbele ya kikao cha Kamati Kuu ili asikilizwe utetezi wake kwa mdomo.
Kwa
maneno yake hayo ni kwamba anakubaliana na na process ya chama na
kwamba anajua atasikilizwa lakini tena wakati huo huo anataka mahakama
imsikilize. Huo ndiyo msingi wa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA kusema kuwa
kuhangaika huko ni sawa na kufanya ‘FORUM SHOPPING’.
Mleta
maombi angeweza kuwa na hoja katika maombi yake iwapo angeona kuna
breach of natural justice kwenye suala lake. Kitu ambacho hakijatokea na
hata yeye kwenye maelezo yake anakiri hivyo.
Uamuzi wa Mahakama Kuu
Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa amesema chama kitaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Hivyo
kikao maalum cha Kamati Kuu kilichopangwa kufanyika kesho Januari 3,
2014, kitafanyika na kitajadili agenda zote (kama zilivyotolewa awali)
na masuala yote yanayohusu uendeshaji wa chama, isipokuwa hakitajadili
na kuamua kuhusu uanachama wa Zitto pekee, hadi Mahakama Kuu
itakaposikiliza ombi lake kesho saa 3 asubuhi.
Kurugenzi ya Habari
No comments:
Post a Comment