Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 6, 2014

Chuji asimamishwa Yanga


Athumani Idd ‘Chuji’
Ally Kamwe na Hans Mloli
HALI si shwari kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga baada ya juzi Jumamosi uongozi wa timu hiyo kuwapa barua za onyo kuhusu utovu wao wa nidhamu na mambo mengine klabuni hapo.

Imeelezwa kuwa, juzi kiungo wa timu hiyo, Athumani Idd ‘Chuji’, alipewa barua ya kusimamishwa klabuni hapo kwa siku zisizojulikana huku nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda, Jerry Tegete na David Luhende wakipewa za onyo kali.
Hata hivyo, uongozi wa Yanga umekuwa na siri kubwa kueleza ni utovu gani wa nidhamu uliosababisha Chuji akasimamishwa na wengine kupewa onyo kali.


TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE) 

Ingawa Championi linafahamu kuwa Chuji alikasirika baada ya kutolewa uwanjani mara baada ya kumalizika kipindi cha kwanza cha mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba na kuondoka moja kwa moja kwenda nyumbani hali ambayo viongozi wameona ni dharau.
Chanzo makini kutoka ndani ya Yanga kimeliambia gazeti hili kuwa, viongozi wa ngazi za juu Yanga walikutana Ijumaa iliyopita, kujadili masuala mbalimbali ya klabu lakini kubwa lilikuwa juu ya wachezaji hao.
Kilisema kuwa kila mchezaji alijadiliwa kulingana na maisha anayoishi klabuni hapo pamoja na nidhamu yake kiujumla ambapo walikubaliana kumsimamisha Chuji, kisha wengine kupewa onyo kwanza kabla ya kuchukua hatua nyingine kubwa zaidi.
“Mipango ilikuwa ni kuangalia tatizo liko wapi Yanga, mara baada ya benchi la ufundi kusafishwa, lengo likawa kurudi kwa wachezaji ambapo tayari Chuji ameshasimamishwa na wengine wamepewa barua za onyo kali.
“Tegete, Niyonzima, Cannavaro na Luhende ndiyo wamepewa hizo barua, wameambiwa wajirekebishe mienendo yao wakiwa Yanga,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.
Championi lilipojaribu kuwatafuta wachezaji hao kuelezea suala hilo, walikana kuwa hakuna taarifa kama hizo na hawajapokea barua kama hiyo ambapo Niyonzima alisema: “Mi sijapokea barua ya onyo lolote, huo ni uongo, kama ningepewa ningekwambia.”CHANZO GPL

No comments:

Post a Comment