Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 18, 2014

DEREVA WA BODABODA ANUSURIKA KIFO

 Pikipiki ikiwa chini ya uvungu wa gari baada ya kuburuzwa 
 Dereva wa pikipiki hiyo Bw Ndiba akihojiwa 
 Ndiba akizunguza na bosi wake mmiliki wa pikipiki hiyo Bw Nassoro Setembo[kulia] 
 Polisi wakiwasili eneo la tukio.
Na Dustan shekidele,morogoro
DEREVA wa boda boda Anthony Kalikana'Ndiba' juzi kati amenusurika kifo baada ya pikipiki aliokuwa akiendesha kugongwa kwa nyuma na kubuluzwa umbali wa mita 200 na daladala eneo la Sido barabara kuu ya Msamvu mjini.

Akisimulia tukio hilo Ndiba alisema" bahati siku na abiri kama ningekuwa na abiria angekufa papo hapo kwani jamaa alikuja kwa  kasi nyuma yangu na kwamba tulipofika hapa Sido  jirani na kanisa la KKKT Mji Mpya amenigonga kwa nyumba na kunirusha bahati mbele kulikuna na gari nikaluka na kuidandia gari ile na kunusulika bila hivyo jamaa angenitoa roho"amesema kwa uchungu boda boda huyo na kuongeza

''Baada ya tukio hilo dereva wa hii daladala alikimbia na mimi kwa hasira nimechukua funguo na kwamba gari haitoki mpaka nilipwe,kifupi mimi ni komandoo sijaumia popote lakini chombo changu  kama unavyokiona kipo chini ya uvungu gari  kimeburuzwa toka pale kanisani mpaka hapa ofisi za Hood"alisema Ndiba
 .
Baada ya muda polisi walifika eneo la tukio na kuchukua pikipiki hiyo pamoja na daladala hiyo ambayo iliendeshwa na dereva mwingine kueleka kituo cha polisi.

No comments:

Post a Comment