Pages

Sunday, January 26, 2014

ESSIEN AHAMIA AC MILAN


article-2545677-1AEFD67400000578-890 634x4171 e3c47
KLABU ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumuuza kiungo Michael Essien kwa AC Milan, timu hiyo ya Ligi Kuu ya England imetangaza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amejikuta anakosa namba kikosi cha kwanza Stamford Bridge tangu arejee Real Madrid alikokuwa anacheza kwa mkopo msimu uliopita na amepewa ruhusa na kocha Jose Mourinho kuondoka.
Taarifa ya Chelsea jana usiku imesema kwamba tayari wamefikia makubalkiano na Milan juu ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ghana. Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment