Kama tungekua nchi za wenzetu tukaanza kuandika kuhusu tatoo na wasanii
basi tusingemaliza leo maana karibia kila msanii ana tatoo na sio moja
tu bali zaidi ya moja.Lil Wayne ana zaidi ya tatoo 300 , Rihanna ana
tatoo 19 ,Miley Cyrus ana tatoo 19 pia huku Bruno Mars akiwa na Tatoo 5 .
Lakini vipi kwa upande wa bongo , Tatoo na usanii au umaarufu vimeanza
kuendana hapa bongo na hii ni list ya wasanii wa bongo wenye tatoos.
Diamond Platnumz
Wema Sepetu
Wema Sepetu ni moja kati ya wasanii wa bongo wenye tatoo nyingi , ana
tatoo kwenye shingo yake , pia ana tatoo yenye maandishi ya kichina
mgongoni yenye maana ya potential kwa kiingireza. pia ana tatoo mkononi
na kwenye bega.
Ney wa Mitego
Ney wa Mitego ni mmoja kati ya wasanii wabishi wanaofanya muziki mgumu
maarufu kama Hip Hop, ambaye amejaribu kubeba dhana hiyo kama msanii
anayetafsirika kimwonekano. Ney wa mitego ameanza kuchora tatoo tokea
mwaka 2002 alipokua kidato cha pili katika shule ya sekondari ya mbezi
beach.Katika mkono wake wa kulia kuna tatoo yenye nanga ya hip-hop ikiwa
na maana kuwa yeye ni mtu mwenye imani na ndoto za kufanikiwa kupitia
muziki huo wa ‘Hip Hop’.‘tattoo’ iliyopo katika mkono wa kushoto ni
nyoka mwenye mabawa(Dragon) ,kiumbe ambacho ni adimu kuonekana duniani.
Elizabeth Michael “Lulu”
lulu naye hayupo nyuma katika kuchora tatoo. kwa upande wa lulu ni
kidogo na wengine kwani yeye ameambua kwenda straight forward na kuweka
ujumbe wa maneno chini kidogo ya shingo lake karibia na bega unaosema
“Only God can Judge Me”.
Jux
Jux ana tattoo mbili. Ya kwanza ipo kifuani na watu wengi wamekuwa
wanasema tatoo hii inafanana na ile ya trey songs lakini ukweli ni kuwa
sehemu ya mwili aliyoichorea ni kama ya Trey Songz lakini fonts na
ujumbe ni tofauti kwani tattoo ya trey songz ameandika ameandika kwa
ajili ya mama yake , mdogo wake wa kiume na bibi yake huku kwa upande wa
jux ukiwa na ujumbe mzito pia lakini hatujajua bado unamhusu nani na
part ya tattoo hiyo inasema “always missing you” na “hope to see you”.
Jux ana tattoo nyingine mkononi maeneo ya bega ikiwa na “Virgo Angel”
kwa kibongo tunaweza kuita mashuke .
Irene Uwoya
Uwoya nae ni kati ya wasanii wakubwa wakwanza kabisa kunyesha tatoo
zake. ana tatoo juu kidogo ya matiti yake yenye alama ya nyayo za paka
au chui.Pia ana tattoo mgongoni iliyoandikwa krrish ikiwa na alama za
nyayo ya mtoto mdogo ambayo ni maalumu kwa mtoto wake Krrish
Ndikumana.Kuna tattoo nyingine zinaonekana kiunoni na miguuni pia.
No comments:
Post a Comment