Pages

Tuesday, January 14, 2014

HATMA YA JAMES MBATIA NCCR-MAGEUZI JUMAMOSI

James Mbatia
 
Chama cha NCCR-Mageuzi kinatarajia kufanya marekebisho ya katiba yake pamoja na kumchagua mwenyekiti wake mpya Januari 18 mwaka huu.
Kwa sasa mwenyekiti wa chama hicho ni James Mbatia ambaye amekiongoza chama hicho kwa takribani miaka 13 tangu mwaka 2000 na atachuana na Charles Makofia, mkazi wa Mpanda mkoani Katavi.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mosena Nyambabe, alisema katiba inayotumika hivi sasa ya chama hicho haina ukomo wa uongozi na kwamba inampa fursa kiongozi kuongoza kwa kipindi kisichokuwa na ukomo kama ataendelea kuchaguliwa.

Nyambabe alisema chama hakiteui mgombea bali kinatoa nafasi kwa kila mwachama mwenye sifa kugombea nafasi yeyote ndani ya chama.

Alisema pamoja na mambo mengine, uchaguzi huo utaambatana marekebisho ya Katiba ya chama.
Watakaochaguliwa na mkutano mkuu Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti Bara, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec).

Kadhalika, Nec itawachagua Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Bara, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mweka Hazina pamoja na baraza la wadhamini.
 

No comments:

Post a Comment