Dr Slaa anaonyesha kabrasha lenye nyaraka mbalimbali ikiwemo mkakati wa mabadiliko 2013, mashtka ya watuhumiwa na nyaraka nyingine muhimu. Sasa Dr. Slaa anasoma mashtaka yote 11 ya Watuhumiwa kama walivyokabidhiwa kwa maandishi
Katibu Mkuu anasema Watuhumiwa wawili yaani Dr. Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba waliitikia wito wa Kamati Kuu lakini aliyehojiwa na Kamati Kuu ni Dr. Kitila Mkumbo pekee ambaye katika utetezi wao walikana kuvunja katiba ya Chama na Kanuni zake.
Katibu Mkuu anasema Dr Kitila Mkumbo alikiri kumfahamu M2 na anamjua fika lakini hawezi kumtaja mpaka awasiliane nae kwanza. Pia Dr Kitila Mkumbo alisema yeye na Mwandishi wa waraka ule walimpa briefing Mh. Zitto Kabwe kwa hiyo alikuwa anaufahamu waraka huo.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Dr. Kitila
Mkumbo alikataa kuzungumzia vifungu vya katiba walivyodai vimevunjwa kwa
madai kuwa tayari wana malalamiko kwa msajili tayari. Aidha Dr. Kitila
Mkumbo alishindwa kuithibitishia Kamati Kuu kwa ushahidi kuhusu madai ya
taarifa ya fedha ambazo yeye na Zitto walishiriki, pia alishindwa
kuonyesha ushiriki wa M/Kiti katika manunuzi ya vifaa mbalimbali vya
Chama zikiwemo pikipiki za Chama.
H...ivyo
Kamati Kuu imeamua kuwavua Uanachama ndugu Samsoni Mwigamba na Dr.
Kitila Mkumbo kuanzia tarehe ya jana baada ya maamuzi ya kikao cha
Kamati Kuu. Maamuzi hayo ni baada ya kunasa mawasiliano mbalimbali ya
Zitto Kabwe na washirika wake akiwemo anayejulikana kwa jina la Chadema
Mpya.
Dr. Slaa anasema malengo ya waraka wa
mabadiliko hayakuwa ya kisiasa tu bali yalikuwa na lengo la kuimaliza
chadema na kuwabomoa Viongozi wa Chama.
Mwisho
Chama kinawatangazia Wanachama wote
na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama shughuli zozote za kisiasa
zitakazoandaliwa na Zitto Kabwe na Washirika wake kwa jina la Chama.
No comments:
Post a Comment