Pages

Wednesday, January 22, 2014

HII NDIO NYUMBA YA MSANII BARNABA......


          
Sio kwamba mastaa wa zamani wa bongofleva hawakuwa wanapata chochote kwenye malipo kutokana na kazi zao bali  imefahamika kwamba mipangilio na matumizi mazuri ya fedha havikuzingatiwa sana kwa baadhi ya Wasanii wachache ambao walibahatika kuzipata
pesa nyingi zilizotokana na mauzo ya kanda na show.
Wasanii wengi wa bongoflevani sasa hivi wameshtukia mchezo ndio maana wengi wao wanaingia kwenye headlines za kuonyesha mali zao kama nyumba na magari siku kadhaa tu baada ya kusikika kwenye chati za bongofleva ambapo hii kwa kiasi kikubwa ni kutokana na malipo ya show zao, wengine mauzo ya nyimbo kwenye miito ya simu, dili za makampuni na ishu nyingine.
Barnaba ni miongoni tu mwa waimbaji wenye talent zao na amekua akifanya showz mbalimbali hata nje ya Tanzania pamoja na kupata dili za mashirika/taasisi mbalimbali na kufanya nao kazi zikiwemo za ubalozi mfano Pepsi, Barclays Bank na wengine kama unavyoweza kuona moja ya stori zake za mwaka 2013.
Screen Shot 2014-01-22 at 1.54.05 AM
Screen Shot 2014-01-22 at 1.54.22 AMBaada ya kuiweka hiyo picha ya nyumba kwenye instagram yake Barnaba aliiambatanisha na hiki hapa chini
Screen Shot 2014-01-22 at 1.38.21 AMBarnaba ameidondosha hii picha ya nyumba yake mwezi mmoja tu baada ya kudondosha picha za gari lake jipya ambalo ni Toyota Mark X.
Screen Shot 2014-01-22 at 1.40.04 AM
Screen Shot 2014-01-22 at 1.40.16 AM
Screen Shot 2014-01-22 at 1.42.05 AM
Credit:-Millardayo.com

No comments:

Post a Comment