skip to main |
skip to sidebar
HOT NEWSS::AFISA UPELELEZI NA MWANAINCHI WAUAWA NEWALA
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linamsaka mtu mmoja ambaye hajatambuliwa
jina kwa tuhuma ya ujambazi na mauaji mwananchi mmoja na afisa upelelezi
wa jeshi hilo wilayani Newala ASP Nurdin Kassim Seif.
Mwananchi mwingine aliayeuawa katika shambulio hilo la kustukiza
ametambuliwa kuwa ni Hamza Msangaluwa aliykufa hapohapo na askari
aliyetambuliwa kwa jina Robert Isaya (33) amejeruhiwa vibaya majani na
amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Newala.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Taarifa
lliyotolewa na jeshi hilo na kusambazwa kwa vyombo vya habari mkoani
Mtwara inasema mtu huyo akiwa na siraha aina ya SMG alifika katika kituo
cha kuuzia mafuta cha camel katika kijiji cha Kiduni nje kidogo ya mji
wa Newala na kuwalazimisha wahudumu kutoa fedha za mauzo yote ya siku
mbili kwa kuwatishia na silaha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo
iliyosainiwa na kaimu kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara Issa Mnilota
jambazi huyo alifanikiwa kupora kiasi cha zaidi ya shs 3,299,180 ndipo
wananchi walipojitokeza kumfukuza hadi umbali wa kiliomita 8 kabla ya
jeshi la polisi kufika katika eneo la tukio.
Taarifa inabaisha
kuwa maofisa wa jeshi la polisi walpofanikiwa kufika katika eneo la
tukio mtuhumiwa akiwa amejificha vichakani alifyatua risasi na kuumuua
raia papo hapo na baadaye kabla ya kumshambulia aliyaekuwa afisa
upelelezi wa wilaya ya Newala na kusababisha kifo chake.
Mwili
wa marehemu Hamza umekwishachukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya
taratibu za mazishi wakati ule wa ASP Nurdin Kasim Seif bado
umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Newala kusubiri taratibu
zingine.
Jeshi la polisi linatoa shukrani kwa wananchi
wilayani Newala kwa ushirikisno waliouonyesha na kuendelea kutoa wito
kwa wananchi mkoani humo kuendelea kushirikiana katika kuwabaini na
kuhakikisha wale wote waliohusika wanatiwa nguvuni.CHANZO STARTV
No comments:
Post a Comment