Pages

Thursday, January 30, 2014

IKULU YA JIJINI DAR ES SALAAM IMETAKA KUFUNGWA KWA MJADALA UNAOHUSU KURUDISHWA KWA MAWAZIRI WANAO DAIWA KUWA MIZIGO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI NA BADALA YAKE IMETAKA WAENDELEE KUFANYA KAZI.


Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu, Bwana Salva Rweyemamu amesema kuendeleza mjadala unaohusu mawaziri mizigo ni kupoteza muda, kwani Rais Jakaya Kikwete Alisha maliza kazi yake.
Aidha Bwana Rweyemamu ameongeza kuwa Rais ndiye  mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri ambao wanawajibu wa kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake, hivyo si sahihi wateule hao kuitwa jina la mawaziri  mizigo ikiwa  Rais ameona wanafaa.
Hayo yamejiri mara baada ya Rais Kikwete kuwarejesha katika baraza la mawaziri baadhi ya Mwaziri ambao walidaiwa kuwa ni mizigo kutokana na udhaifu katika utendaji  kazi wao,
baadhi ya mawaziri  hao ni pamaja na Christopher Chiza, waziri wa kilimo chakula na ushirika, Dr. Shukuru Kwambwa, waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi  Hawa Ghasia na manaibu wake Kasimu Majaliwa, na Agrey Mwanri katika wizara ya nchi, ofisi ya waziri mkuu (Tamisemi).

No comments:

Post a Comment