Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 13, 2014

JANA TULIPATA AJALI MLIMA KITONGA,NAMSHURU MUNGU KWA KUTUNUSURU NA KUTUWEKA HAI

Hii ni Bampa ya pembeni ikiwa imetolewa kutokana na presure kali ya upepo baada ya tairi kupasuka

dereva msaidizi akifungua nati za matiri illi kuweza kutoa tairi iliyopasuka


Hii ndio tairi iliyopasuka na kusababisha gari kupoteza mwelekeo

Hii ni sehemu ilipasuliwa na presure ya upepo baada ya tairi kupasuka










Ashukuriwe baba Mungu muumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa neema zake na baraka tele juu yangu na abiria wenzangu.
Jana nilikuwa safarini kutokea mkoani Mbeya kuja Jijini Dar es salaam kwa basi la Ndenjela Luxury Coach,Tulianza safari yetu vizuri na salama tukiwa na furaha na matumaini mengi ya kufika salama kutokana na umakini na mwendo mzuri wa derva wetu.
Ilipofika saa Tano na nusu mchana tukiwa eneo lenye milima mikali sana mkoani Iringa,Eneo hilo maarufu kama mlima kitonga Basi letu lilipata Pancha tairi la nyuma kulia.
 Ndipo basi likaanza kwenda mrama huku likuyumba sana LAKINI KWA UWEZA WA JEHOVA NA NGUVU ALIZOPEWA DEREVA WETU NA MUNGU BABA,Dereva aliweza kujitaidi kulimudu gari vizuri na hatimaye kuweza kulipeleka pembeni na kupaki.
Tunashukuru mungu hakuna mtu aliyeumia wala kupata majeraha bali mshtuko tu wa tairi kupasuka kwa nguvu.Tulisaidiana na madereva kwa takribani masaa mawili na hatimaye kufanikiwa kubadili tairi nyingine na kuendelea kwa safari yetu na hatimaye kufika salama Jijini dar mida ya saa Nne Usiku.Admin wenu wa Dj sek niko salama na tunaendelea kuhabarishana.

No comments:

Post a Comment