Kamishna
wa Polisi jamii nchini, CP Mussa Alli Mussa, akitoa neno mbele ya
askari na maofisa katika kikao cha utendaji kazi kilichofanyika jana
jijini Dar es salaam(picha na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi )
…………………………………………………………………..
Na Demetrius Njimbwi na Alexander Mpeka, Jeshi la Polisi
Na Demetrius Njimbwi na Alexander Mpeka, Jeshi la Polisi
Kamishna
wa Polisi Jamii Nchini, (CP) Mussa Alli Mussa, amewataka maofisa wa
Polisi pamoja na askari kote nchini, kuhakikisha wanafanya kazi zao
katika misingi ya uwazi na usasa, dhana itakayosaidia uenezi wa Polisi
jamii/ulinzi shirikishi katika kupambana na matukio ya uhalifu na
wahalifu.
Kauli
hiyo ameitoa jana wakati alipokutana na baadhi ya watendaji wa Jeshi la
Polisi katika wilaya ya kipolisi ya Ilala, katika kikao cha pamoja
kuhusiana na utendaji wa Polisi katika dhana ya Polisi jamii na namna
ambavyo Jeshi hilo linavyoweza kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa
pamoja na kushirikiana na wananchi na jinsi wanavyoshirikishwa.
Kamishna
Mussa, aliongeza kuwa, tangu kuanzishwa kwa Polisi jamii/ulinzi
shirikishi, mafanikio makubwa yameweza kufikiwa kwani mpaka sasa makundi
kadhaa ya uhalifu yameweza kugundulika na kuchukuliwa hatua ikiwamo
kuangamizwa ikiwa pamoja na wahusika kuchukuliwa hatua kali za
kisheria, alisema.
Hata
hivyo, Kamishna Mussa, aliwataka wananchi kuwathamini na kuwapa
ushirikiano maofisa wa Polisi/Polisi Kata pamoja na vikundi vya Ulinzi
Shirikishi hatua ambayo itasaidia kukabiliana na matukio ya uhalifu
katika maeneo mbalimbali na kuifanya jamii kuishi kwa amani pasipo
kuwepo kwa matukio hatarishi.
Kwa
upande wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lazaro Mambosasa,
alisema kuwa, Jeshi l Polisi limejipanga katika kukabiliana na aina
zote za uhalifu na kwamba alitamuonea ama kumdhurumu mtu yeyote katika
kusimamia na kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mambosasa,
ameongeza kuwa, kila askari katika nafasi yake anawajibu wa kuhakikisha
kuwa, jamii inaondokana na uhalifu pamoja na matishiona huku akiwataka
maofisa na askari kuwa na utayari katika kutoa huduma bora kwa wananchi
kwa kuzingatia dhana ya Polisi Jamii/Ulinzi shirikishi, alisema.
No comments:
Post a Comment