Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 29, 2014

KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI, PAC, IMEPANGA KUZIKUTANISHA KWA PAMOJA, WIZARA YA FEDHA PAMOJA NA WIZARA YA ELIMU WAKATI IKIPOKEA TAARIFA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI ILI KUJUA MATUMIZI YA FEDHA ZA MAREJESHO YA RADA ZILIVYOTUMIWA.


Akizungumza  jana  Jijini  Dar es Salaam  Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe alisema kuwa wanatarajia kupokea taarifa hiyo ili  kujihakikishia kama matumizi hayo yalikuwapo au kulikuwa na ulaghai wa aina yoyote.
Aidha amesema Kwa sasa ni mapema kuanza kufikiri kwamba fedha hizo  hazikutumika kama  inavyotakiwa, lakini kama kuna ujanja wowote ulifanyika utabainika ndio maana wametaka kukutana na wizara ya Fedha( CAG)pamoja na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ili kupata majibu ya papo kwa papo. 
Novemba mwaka jana Serikali ilianza kusambaza vitabu milioni 19.4 kwa shule za msingi nchini, ambavyo ilielezwa kuwa vimenunuliwa kwa chenji ya rada na asilimia 75 ya fedha hizo zimetumika kununulia vitabu hivyo na asilimia 25 zitatumika kununulia madawati.

No comments:

Post a Comment