Saa tano
asubuhi leo zimetoka taarifa za abiria wapatao kumi kurushwa ghafla
baharini baada ya boti waliyokua wakisafiria kutoka Pemba kwenda Unguja
kupatwa na dhoruba ya upepo mkali kwenye eneo hatari la Nungwi huku
maelezo ya abiria waliohojiwa yakisema watu hao ilibidi waachwe ili boti
nzima isizame lakini wakatupiwa maboya ya kujiokoa.
msemaji
wa Polisi Zanzibar ambae anasema ‘ni kweli kuna boti ya Kilimanjaro II
iliondoka Pemba kwenda Znz saa mbili na dakika 20 asubuhi ikiwa na
abiria 369 Wakubwa, abiria wadogo 60 na mabaharia Wanane na kwamba boti
hii ilipofika kwenye eneo hatari la Nungwi saa nne na dakika 15 ilipata
dhoruba kutokana na upepo mkali’
‘Baada ya
muda kidogo wakati wa tukio hili kuna baadhi ya abiria walichukua life
jacket 5 na kuzitupa baharini bila maelekezo ya nahodha au bila kupata
amri kutoka kwa Wafanyakazi wa meli hiyo ambapo baada ya tukio hili boti
iliendelea na safari na kufika salama na abiria wake Znz saa tano na
dakika 50′
Kuhusu
taarifa za watu 10 kurushwa baharini wakati upepo mkali ulipotokea,
Polisi wanasema ‘hakuna mtu yeyote aliedondoka baharini na hizi taarifa
ni kwa mujibu wa Captain wa boti hii N. Abubakar’.NA MILLADAYO
No comments:
Post a Comment