Bingwa wa michezo ya all African Games mwaka 1973 ndg Kipchoge Keino (KULIA) wa Kenya ambaye ndiye mkimbizaji wa kifimbo cha malkia akiwa na mmliki wa blog ya Lenzi ya michezo |
Watoto wa shule ya Filbert Bayi wakicheza ngoma |
JKT Mgulani |
MJUMBE wa
Baraza la Michezo ya Jumuiya ya Madola, Kipchoge Keino ameitaka
serikali kuweka mipango dhabiti ya kuendeleza michezo.
Keino
ambaye ndiye mkimbizaji wa kifimbo cha malkia aliyasema hayo wakati
alipotua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kupokele na
viongozi wa serikali na kamati ya Olmpiki Tanzania.
“Tanzania
ina vipaji na hili nalijua kwani nilikuwa na Filbert Bayi kwenye
mashindano mbalimbali ya kimataifa hivyo mikakati ikiwekwa ya kuendeleza
vipaji nchini itapata medali nyingi kwenye mashindano ya kimatifa”’
alisema Keino ambaye alishawahi kuwa bingwa wa mashindano ya Afrika (all
African Games)
Kifimbo
hicho kiliktua nchini kikitokea nchini Rwanda na kukabidhiwa kwa Rais
wa Kamati ya Olympiki Tanzania Rashid Gulam na leo kitakimbizwa katika
mitaa na barabara kadhaa za jijini la Dar es Salaam na Baadae
kitapelekwa Ikulu kabla ya kwenda Zanzibar .
“Kifimbo
cha Malkia kesho kitakuwa hospitali ya Muhimbili kwenye wodi ya watoto
wenye ugonjwa wa saratani ili wacheze nacho, baadae kitapelekwa Uwanja
wa Taifa ili watu wakione na kupiga picha, baadae kitakimbizwa katika
barabara ya Nelson Mandela kikifika TAZARA kitapitia barabara ya Nyerere
kurudi mjini kupitia Gerezani baadae kitapelekwa Ikulu ambako
kitapokelewa na Rais Jakaya Kikwete:, alisema Jabir ambaye ni katibu wa
kamati Maalum ya TOC”, alisema
“Kikiwa Zanzibar kitakimbizwa Mji Mkongwe na sehemu nyingine za Historian a baadae kitapelekwa Ikulu ya Zanzibar”, alisema
Pia Jabir
aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi
kukimbiza kifimbo hicho kwani watanzania wana historia ya kuwa wakarimu.
No comments:
Post a Comment