Pages

Wednesday, January 8, 2014

KIIZA AFICHUA KILICHOMFUKUZISHA BRANDTS YANGA


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza amesema kuwa aliyekuwa kocha wao mkuu, Ernest Brandts amejitakia kufukuzwa kwenye timu hiyo inayojiandaa na Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.
Hiyo ni siku chache tangu uongozi wa timu hiyo kutangaza kulitimua benchi zima la ufundi lililokuwa linaongozwa na kocha huyo na msaidizi wake Fred Minziro na kocha wa makipa Mkenya, Razack Siwa kwa kilichodaiwa kushindwa kazi na kuzidiwa uwezo na kikosi hicho.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kiiza alisema kuwa siku zote Yanga wanataka matokeo mazuri ya ushindi na si kingine, hivyo kocha huyo alikuwa akipanga timu kwa mazoea.
"Ujue kocha wetu (Brandts) amejitakia mwenyewe kufukuzwa kwenye timu, ameshindwa kujua Wanayanga wanataka nini, wao wanataka matokeo mazuri ya ushindi si kingine.

 
"Ninaamini kama timu ingekuwa inapata matokeo katika mechi zake, basi angeendelea kubaki kuifundisha Yanga, si kocha mbaya ni mzuri tena ana uwezo mkubwa wa kufundisha, lakini hilo la matokeo ndiyo limemwondoa.
"Hakuwa makini katika kupanga timu itakayopata matokeo mazuri kwenye mechi, alikuwa akipanga timu kutokana na mazoea. Aliogopa baadhi ya wachezaji kwa kuwapanga kikosi cha kwanza katika mechi wakati uwezo wao ni mdogo,'' alisisitiza mchezaji huyo bila kutaja majina ya wachezaji ambao uwezo wao mdogo.
Kiiza ambaye pia aliwahi kutofautiana waziwazi na Brandts aliongeza: "Mashabiki wa Yanga wanataka matokeo mazuri, sichagui kocha wa kufanya kazi naye, yeyote yule nitampa ushirikiano

No comments:

Post a Comment