THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia Salamu za Rambirambi Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, Mheshimiwa Damian Zefrin Lubuva kufuatia kifo cha Mke
wake, Mama Martha Peter Lubuva kilichotokea tarehe 17 Januari, 2014
katika Hospitali ya Apollo iliyoko New Delhi nchini India alikopelekwa
kwa matibabu akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.
“Nimeshtushwa,
nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mke
wako, Mama Martha Peter Lubuva aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya
Apollo nchini India akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Kisukari ambao
umesumbua kwa muda mrefu”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake za
Rambirambi.
Rais
Kikwete amesema anatambua fika machungu ambayo hivi sasa wanapitia
watoto na Familia nzima ya Mheshimiwa Damian Zefrin Lubuva kutokana na
kuondokewa na Mama yao Mzazi na Kiongozi muhimu wa Familia, lakini
amewaomba wawe watulivu na wavumilivu, lakini muhimu zaidi wawe na moyo
wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao.
“Ninawahakikishia
kuwa niko pamoja nayi katika kuomboleza msiba huu mkubwa na namuomba
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi
Roho ya Marehemu, Mama Martha Peter Lubuva kwa kutambua kuwa yote ni
Mapenzi yake Mola”.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Januari, 2014
No comments:
Post a Comment