Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
Ikulu yafanya uteuzi, kuhamisha Makatibu Tawala
Wamo Chambo, Dk. Ndunguru
Wamo Chambo, Dk. Ndunguru
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, leo anakutana na vyombo vya habari
Ikulu jijini Dar es Salaam kwa kile kinachotarajiwa kutangazwa kwa
mawaziri wapya.
Uwezekano
huo unatokana na taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana ikieleza kuwa
Balozi Sefue ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Mawaziri atazungumza na
wanahabari katika kikao hicho kinachotarajiwa kufanyika wakati wowote
leo.
“Katibu
Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Balozi Ombeni Sefue ambaye
ni Katibu wa Baraza la Mawaziri, leo, Jumapili, Januari 19, 2014,
atazungumza na waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika Ikulu,
Dar es Salaam.” Ilisema taarifa hiyo, iliyosainiwa na Mwandishi wa
Rais, Salva Rweyemamu.
Matarajio
ya wengi yalikuwa Rais Jakaya Kikwete angetangaza baraza la mawaziri
wiki hii ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na mawaziri wanne
walioshinikizwa na Bunge kujiuzulu, kufuatia kushindwa kusimamia
majukumu yao kwenye Operesheni Tokomeza Ujangili iliyosababisha vifo na
uharibifu wa mali za watu.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGIIII MOTOMOTO(USIPITWEEEEE)
Waliojiuzulu
ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David, Waziri wa
Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki , Waziri wa Mambo ya
Ndani Dk John Nchini, na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Shamsi Vuai Nahodha. Pia alitarajiwa kutangaza Waziri wa Fedha kuchukua
nafasi ya marehemu Dk William Mgimwa, aliyeaga dunia Januari mosi mwaka
huu.
Mwanzoni
mwa mwezi huu kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari
zikipendekeza baadhi ya sura zinazotarajiwa kuingia katika baraza hilo.
Hata hivyo, ukweli utajulikana leo baada ya Katibu Mkuu Kiongoza kutangaza rasmi.
Kuna
wasiwasi kuwa huenda Rais akawabadilisha baadhi ya mawaziri wanaodaiwa
kuwa mizigo, baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuwataja na
kupendekeza wahojiwe na Kamati Kuu (CC) ya chama.
Wizara zinazolalamikiwa ni ya Maji, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.
Aidha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Dk. John Ndunguru, anakwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma.
Taarifa
ya Ikulu iliyotolewa Dar es Salaam jana ilisema uteuzi huo pia
umemhamisha Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sipora Liana kwenda Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa (Tamisemi) na nafasi
yake kuchukuliwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Iddi.
MAKATIBU WAPYA
Makatibu
Tawala wapya wa mikoa mitano ni Wamoja Dickolangwa (Iringa) Abdallah
Chikota (Lindi), Symthies Pangisa (Rukwa), Alfred Luanda (Mtwara) na
Jackson Saitabau ( Njombe).
WALIOHAMISHWA
Beatha
Swai aliyekuwa Pwani amehamia Tamisemi, Benedict Ole Kuyan zamani Tanga
sasa Mara, Salum Chima wa Rukwa anayekwenda Tanga, Mgeni Baruani
zamani Njombe na sasa anakwenda Pwani. Uteuzi na uhamisho huo ulianza
rasmi jana kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment