Pages

Wednesday, January 29, 2014

Kony aomba msamaha kwa serikali ya Uganda

Joseph Konyi kiongozi wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army (LRA) la nchini Uganda, ameiandikia ujumbe serikali serikali ya nchi hiyo akiomba msamaha na maelewano ya amani kwa ajili ya kumaliza uasi nchini. 
“Nataka kuwafahamisha watu wa Uganda kwamba, sisi wanachama wa kundi la (LRA) tumeungana pamoja kwa ajili ya kurejesha amani iliyokumbwa na vita vya muda mrefu na serikali ya Rais Museven.” Umesema ujumbe wa Kony. Kony ameongeza kama ninavyo nukuu: 
“Tupo tayari kwa ajili ya kuomba msamaha na kusamehi na pi kudumisha amani na kumaliza vita hivi vilivyoathiri nchi za eneo la Maziwa Makuu za Afrika.” 
Mwisho wa kunukuu. Mazungumzo kati ya serikali ya Unganda na kundi la waasi wa Lord's Resistance Army (LRA), yaliyokuwa yakiendelea mjini Juba, Sudan Kusini, yalikwama baada ya Joseph Konyi kukataa kutia saini makubaliano ya mwisho mwaka 2008. 
Joseph Konyi kiongozi wa kundi hilo la waasi wa (LRA) anaaminika kujificha nchini Kongo DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

No comments:

Post a Comment