KAMPUNI YA RELI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YA KUAHIRISHA SAFARI YA TRENI YA
ABIRIA KWENDA BARA HADI JUMAPILI JANUARI 05, 2014
Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi
kwa jumla kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni
ya abiria iliyopangwa kuondoka jana Ijumaa Januari 03, 2014 saa 3
usiku imeahirishwa hadi kesho Jumapili Januari 05 Machi 16, 2013,
saa 3 usiku.
Taarifa
imefafanua kuwa kutokana na mvua kunyesha mkoani Dodoma na mikoa jirani
eneo kati ya stesheni za reli ya kati za Gulwe na Godegode zimejaa
maji na kufunika njia ya reli mkesha wa mwaka mpya wa 2014!.
Tokea
juzi Januari 02, 2014 Wahandisi na mafundi wa kampuni za TRL na Rahco
kwenye sehemu husika wakifanya tathmini na kusimamia ukarabati wa
maeneo mawili reli yaliyoharibika.
Kwa
mujibu Mkururgenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu
anayeongozwa kikosi kazi cha kukarabati amesema kazi ya ukarabati
inafanywa usiku na mchana kuona huduma zinaanza mapema iwezekanavyo
ikiwemo huduma ya usafiri wa treni za abiria uliopangwa kuanza tena
hapo kesho Jumapili Januari 05, 2014.
Kutokana
na dharura hii treni za kutoka Mpanda, Kigoma na Mwanza kuja Dar
zimebadilishiwa muda na siku ya kuondoka hivyo basi, badala ya kuondoka
jana Ijumaa Januari 03, 2014 sasa zitaondoka kesho Jumapili Januari 05,
2014 saa 2 asubuhi.
Aidha
taarifa hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati
na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote
utakaojitokeza..
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal Mafikiri.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Januari 04, 2014
No comments:
Post a Comment