Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazin Bw Mahmoud Mgimwa akifungua mashindano hayo |
Mmoja kati ya wana vyuo kutoka Mufindi akizungumza na vijana .
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazin Bw Mahmoud Mgimwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazin Bw Mahmoud Mgimwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazin Bw Mahmoud Mgimwa akionyesha uwezo wake katika soka kabla ya kuzindua mashindano hayo
JUMLA
ya timu 5 za jimbo la Mufindi Kaskazin zajitosa kuwania kombe
la Mbunge Mahmoud Mgimwa ( Mgimwa Cup) katika tarafa ya Sadani .
Timu hizo ni kutoka kijiji cha Ikweha,Ugenza,Ilangamoto, Sinai na
Ukeremi ambazo zote zimepata kutambaana kuondoka na ubingwa katika mashindano hayo.
Akifungua pazia la mashindano haya wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2014 jana katika uwanja wa kijiji cha Ugenza kata ya Ikweha, Mgimwa alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha kasi ya maendeleo kwa vijana kupitia michezo .
Alisema kuwa mashindano hayo yameanzishwa na kusimamiwa na
shirika la Mgimwa foundation pamoja na umoja wawanafunzi walio maliza vyuo vikuu
wilayani katika wilaya ya Mufindi (MUYOWIRUDE)
Mgimwa
alisema nidhamira yake na viongozi anaoshirikiana nao kuhakikisha vijana katika
jimbo lake wananufaika kwa kupitia michezo kasi ya maendeleo kwa jimbo hilo kupitia vijana inazidi kukua zaidi
Mbunge huyo alisema zawadi mshindi wa
kwanza atapata jumla ya Track suti 16 zenye thamani ya shiringi
480,000/=pamoja na mipira miwili yenye thamani ya shilingi 150,000 na kufanya zawadi zote kuwa na jumla ya Tshs. 630,000
Huku
mshindi wa pili atazawadiwa seti ya Jezi yenye
thamani ya shilingi 250,000/=pamoja na mipira miwili ya Shilingi 150,000
na kufanya zawadi zote kufikisha kiasi cha Shilingi 400,000 wakati mshindi wa tatu atapata mipira miwili yenye thamani
ya shilingi 150,000
Kabla ya mashindano hayo mbunge huyo alikabidhi seti ya Jezi kwa
kila timu pamo na mpira mmoja wa mazoezi.
Pia alikabidhi mipira miwili kwa waamuzi wa
mashindanohayo kwa ajili ya kushindania sambamba na hilo pia Mgimwa alisema atatoa zawadi
mbali mbali kama .
Kwa mfungaji wa goli la kwanza katika mashindano
hayo atapata shilingi 20,000 mchezaji mwenye nidhamu atapata shilingi
30,000 na timu yenye nidhamu itapata shilingi 50,000 huku mchezaji bora
atapata shilingi 50,000
Hivyo
aliwataka vijana kwa kupitia mashindano hayo kuhakikisha wana
wasikiliza vema watakapo kuwa wakipatiwa mafunzo ya stadi za
maisha kwakupitia wawezeshaji toka shirika la (MUYOWIRUDE).
Ambao wataenda sambamba na michezo hiyo kwani
watapa kujifunza bure elimu mbali mbali .
Kiongozi wa wanafunzi hao Marko Shayo alisema wao watatoa elimu yanamna yakujikinga na maambukizi ya Ukimwi,Elimu ya
Ujasiriamali kwa kutumia zilizopo katika jimbo lao.CHANZO FRANSIS GODWIN
No comments:
Post a Comment