Zaina Ramadhan ‘Nandi’.
MSANII wa Kundi la Kaole Sanaa, Zaina Ramadhan ‘Nandi’ anasumbuliwa na ugonjwa wa mifupa akidai kuvunjika pingili za mgongo kisha kushindwa kutembea na kufanya kazi zake za sanaa na nyinginezo.
Akipiga
stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Nandi alisema kuwa alianza
kuumwa baada ya kupata hitilafu mwaka 2012 alipokuwa akitoka Chuo cha
Sanaa pale Lego, Ubungo jijini Dar.
“Sikujua
kilichonipata, nikaenda nyumbani wakanichua na mafuta ya asili ambayo
yalinisaidia kidogo lakini tatizo lilizidi kuwa kubwa. Nikiwa nyumbani
mama aliniomba nimsaidie kubeba vyombo lakini nilishindwa kuinua beseni
baada ya kuinama na pingili za mgongo zikavunjika,” alisema Nandi.
Baada ya hapo, Nandi alisema alikwenda
Hospitali ya Mwananyamala, Kinondoni jijini Dar ambapo alimuona daktari
akamuandikia dawa za kutuliza maumivu na kumhamishia Muhimbili kwa
uchunguzi zaidi.
Nandi amewahi kucheza filamu mbalimbali ikiwemo Yatima, Jua la Kiama, Kuzaa si Kupata na nyingine nyingi.
Kwa aliyeguswa na tatizo la msanii huyo na mwenye nia ya kumsaidia, awasiliane naye kwa namba 0684501177.
No comments:
Post a Comment