Pages

Tuesday, January 28, 2014

MHE. BALOZI BEGUM K. TAJ AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO HISPANIA

 Tarehe 21 Januari, 2014 Mhe. Begum K. Taj, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Hispania mwenye makazi yake Paris Ufaransa aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa  Mtukufu Juan Carlos I,
Mfalme wa Hispania. Hafla hii ilifanyika kwenye kasri ya mfalme (Zarzuela
Palace) Madrid Hispania.
  Pichani Mhe. Balozi Begum K. Taj akimkabidhi Mtukufu Juan Carlos I, Mfalme wa Hispania, Hati zake za Utambulisho.
Mhe. Balozi Begum K. Taj pamoja na mabalozi wengine waliowasilisha hati zao wakimsikiliza kwa makini Mtukufu Juan Carlos I, Mfalme wa Hispania. Jumla ya Mabalozi 14 waliwasilisha hati zao siku hiyo.

No comments:

Post a Comment