Pages

Friday, January 24, 2014

Milipuko mikubwa yatikisa Cairo


Mlipuko umetokea wakati wa kuadhimisha siku ya kuondolewa mamlakani kwa Hosni Mubarak
Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka nje ya makao makuu ya polisi katika mji mkuu wa Misri, Cairo na kuwauwa zaidi ya watu wanne huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa kulikuwa pia na ufyatulianaji wa risasi.
Na wakati wafanyikazi wa kutoa huduma za dharura walipokuwa wakienda katika eneo la tukio, polisi walionekana wakilia nje ya jengo hilo.
Mlipuko huo umeharibu jengo la makavazi ya sanaa ya kiislamu lililopo karibu na eneo hilo.
Baadaye kulitokea mlipuko mwingine katika kituo cha basi eneo la Dokki na kusababisha vifo zaidi.
Duru zinasema kuwa watu wawili waliojihami kwa bunduki waliwashambulia walinzi katika jengo hilo la polisi.
Kituo cha televisheni cha Serikali kimesema kuwa milio ya risasi ilisikika mara tu baada ya mlipuko huo.
Moshi ulionekana ukifuka juu ya majengo katikati mwa mji na picha za televisheni zilionyesha uharibifu mkubwa wa majengo hayo.
Zaidi ya ambulansi 30 zimepelekwa eneo hilo kushughulikia waathiriwa. Mlipuko huo umetokea siku ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kupinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Hosni Mubarak.

No comments:

Post a Comment