Uongozi
wa Young Africans SC umepata warithi wa nafasi tatu za benchi la ufundi
(Charles Boniface Mkwasa, Juma Pondamali na Dr. Suphian Juma), huku
wakiendelea na mchakato kumpata kocha mkuu ambaye atachukua nafasi ya
mholanzi Ernie Brandts aliyesitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka
2013.
Charles
Boniface Mkwasa “Master” aliyekua kocha mkuu wa timu ya Ruvu Shooting
katika mzunguko wa kwanza anachukua nafasi ya aliyekua kocha msaidizi
Fred Felix “Minziro” ambaye muda wake umemalizika mwishoni mwa mwaka
2013.
Mkwasa
ambaye aliichezea Young Africans miaka ya 80′s kwa kiwango cha hali juu
pia alishawahi kuwa Kocha Mkuu/Msaidizi kwa kikosi cha Jangwani kwa
vipindi tofauti jambo ambalo linamfanya asiwe mgeni katika mitaa ya
Twiga na Jangwani.
Kocha
wa makipa wa timu ya Taifa Tanzania “Taifa Stars” Juma Pondamali
“Mensah” anachukua nafasi ya aliyekua kocha wa makipa mkenya Razaki Siwa
ambaye pia alisitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.
Pondamali
golikipa aliyeichezea Yanga miaka ya 80′s kwa kwa kiwango cha hali ya
juu hata kufikia kuwa katika kikosi cha Tanzania kilichoshiriki
mashindano ya Mataifa Afrika nchini Nigeria mwaka 1980, sio mgeni katika
timu ya Young Africans kwani awali alishawahi kuwa kocha msaidizi kwa
vipindi tofauti.
Dr
Suphian Juma anachukua nafasi ya Dr Nassoro Matuzya ambaye pia
alisitishiwa ajira yake mwishoni mwa mwaka 2013 pamoja benchi la Ufundi.
Mara
baada ya kuwapata viongozi hao watatu wa Benchi la Ufundi kikosi cha
Young Africans kesho kitaanza mazoezi jioni katika Uwanja wa Bora
Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja
na mashindano ya Kimataifa huku kocha Mkwasa akiongoza benchi hilo la
Ufundi mpaka atakapopatikana kocha mkuu ambaye watafanya watafanya kazi
kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment