Pages

Wednesday, January 22, 2014

MWAKA WA MAJANGA KWA WEMA SEPETU..!! KUPELEKWA TENA MAHAKAMANI KUJIBU KESI ILOYOWAHI KUISHA NA SASA IMERUDI TENA..!!


MENEJA wa hotel ya Mediteranian iliyoko Kawe Beach jijini Dar es salaam aliyepigwa makofi na kutukanwa na beautiful Onyinye wa bongo movies Wema Isack Sepetu amesema kuwa ameshampata wakili mkubwa wa kumsaidia katika rufaa ya kesi yake na kwamba sasa kesi hiyo itasimamiwa kwa ushirikiano na mabosi wake
Akiongea na Swahilitz meneja huyo ambaye hakuridhika na hukumu ya Wema kutoa laki moja na kumaliza kesi katika mahakama ya mwanza ya Kawe chini ya mheshimiwa Hakimu Bernice Ikanda.
"Unajua mara ya kwanza niliambiwa siwezi kushindanan na Wema kutokana na mwanja mkubwa aliokuwa nao lakini nilimuomba Mungu anisaidie kwa hilo kwasababu kwa Mungu hakuhitaji hela, nimesimama kidete na kumuomba Mungu na sasa kesi nairudisha upya kwani wakili niliyempata na wa kizito na ni wa uhakika" alisema meneja huyo.
Alifafanua kuwa katika rufaa yake atakuwa sambamba na wakili huyo pamoja na wamiliki wa hotel ya Mediteranian ambao kwa pamoja wameahidi kuhakikisha suala hilo linapatia ufumbuzi yakinifu.
Wema alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake na Mheshimiwa Hakimu Bernice Ikanda na kudaiwa kufanya  vurugu kushambulia na kumpiga makofi na kumtukana bwana Goodluck Kayumbu. Hata hivyo katika katika kujitetea alidai kuwa yote yalifanyika kwasababu ya pombe na sio kwa masudi
Hatua ya bwana Kayumbu kukimbilia rufaa katika kesi ambayo ilishamalizika ni pigo la pili kwa Wema ndani ya mwaka huu kwani hivi karibuni imeelezwa kuwa alikumbwa na mkosi baada ya mahakama ya Ilala kuamuru anyang'anywe gari lake la kifahari aina ya Audi Q7 lenye usajili wa T973 BUJ na kukabidhiwa kwa mmiliki wa gari hilo.

No comments:

Post a Comment