Taarifa zilizochapishwa kwenye ZanziNews.com jioni ya jana zinasema kuwa juhudi za wananchi na vyombo husika mpaka sasa
zimefanikiwa kuwapata wananchi wanne wakiwa hai na miili ya watu watano
walioaga dunia (wanawake wawili na wanaume watatu). Miili ya maiti
imehifadhiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja. Serikali itaandaa
utaratibu wa kawaida kwa maiti kuzikwa ama kupewa jamaa zao. Kapteni Nassor Abubakar Khamis ameshikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Zoezi la uokozi limesitishwa katika eneo la ajali kutokana na giza hadi hapo leo asubuhi.
Kutokana
na kuwepo kwa taarifa za kukanganya ambapo baadhi ya abiria wanadai
kutokuwaona ndugu zao 7 kwa kuwa walianguka kwenye maji baada ya MV
Kilimanjaro kukumbwa na dhoruba na hadi sasa hawajaonekana; Huku nahodha
wa boti hiyo akikaririwa kusema kuwa hakuna yeyote aliyeanguka ama
kuachwa
katika
eneo la mkondo wa maji wa Nungwi; Wakati kamishna wa polisi Zanzibar
Hamdan Makame amesema zipo ripoti ambazo hazijathibitishwa kuhusu watu 4
waliolazwa katika kituo cha afya cha Nungwi baada ya kuokolewa;
Blog ya Zanzibar Islamic News inaripoti kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman amsesema tayari kundi la wazamiaji tayari limekwenda katika eneo la ajali. Waziri Seif amesema kamati ya ulinzi na usalama imekutana mchana huu na kujadili tukio hilo kabla ya kuelekea eneo la tukio kushirikiana na wataalam wengine kuwatafuta watu hao.Nalo Jeshi la polisi Zanzibar kwa kushirikiana na Jeshi la polisi Makao makuu Dar es salaam wametuma helkopta katika eneo la tukio ili kubaini watu ambao wanadaiwa kuzama katika eneo hilo.Mkurugenzi wa Usafiri wa Baharini (ZMA) Mhandisi Abdi Maalim amesema mabaharia walianza kazi ya kuwatafuta watu wanaosadikiwa kuzama majira ya alasiri jana kwa kushirikiana na mabaharia wa kujitolea.Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai Zanzibar DCI Yussuf Ilembo amesema uhakiki wa majina ya wahanga bado unaendelea ili kupata majina yao na umri wao kwa vile kuna meli mbili zilisafiri kwa wakati mmoja.
Taarifa
zilizotolewa mchana wa leo kupitia vyombo mbalimbali vya habari
zilisema kuwa mnamo wa majira ya saa tano adhuhuri ya jana, boti ya MV
Kilimanjaro II mali ya kampuni ya Azam Marine, ilipatwa na dhoruba
katika eneo la Nungwi wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja na kwamba
abiria wapatao kumi hivi walianguka majini na kutupiwa maboya ya
kujiokoa.Msemaji
wa Polisi Zanzibar amekiri kutokea kwa dhoruba hiyo iliyosababishwa na
upepo mkali ulioipiga boti hiyo iliyokuwa na abiria 369, watoto 60 na
mabaharia 8 na kisha baadhi ya abiria kutupa maboya matano baharini bila
ya maelekezo kutoka kwa nahodha wala mabaharia wa boti hiyo.
Lakini
msemaji huyo amekaririwa akitamka kuwa kwa mujibu wa nahodha Aboubakar
wa chombo hicho, hakuna mtu yeyote aliyedondoka ama kuachwa katika eneo
la dhoruba na boti ilifanikiwa kutua nanga salama u salmin katika
bandari ya Zanzibar mwendo wa saa sita kasoro mchana.
No comments:
Post a Comment