Pages

Thursday, January 23, 2014

Ndikumana aipaisha Burundi Chan

ndiku1 f5910
Ushindi huo umeifanya Burundi kukaa kileleni kwenye kundi hilo baada ya kuwa na pointi nne, sawa na Gabon iliyozidiwa mabao ya kushinda, wakati Mauritania, watakuwa wameaga michuano hiyo. (HM)
Mechi hiyo ilikuwa ngumu sana, Mauritania wakifunga bao katika dakika ya pili tu kupitia Ely Cheikh Voulany baada ya makosa ya mabeki kabla ya Burundi kusawazisha dakika 10 baadaye.
Baadaye Burundi walipata penalti baada ya Claude Ndarusanze kuangushwa ndani ya boksi na Ndikumana alipiga mkwaju huo na kupoteza na kufanya mapumziko matokeo kuwa 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, kwenye dakika 61, Christophe Nduwarugira (pichani) aliipigia Burundi bao la kuongoza kabla ya Mauritania kusawazisha dakika tisa baadaye na kufanya matokeo kuwa
2-2.

Wakati wengi wakiamini kwamba mchezo huo utamalizika kwa sare, Ndikumana alifunga moja ya mabao bora kwenye mashindano hayo baada ya shuti lake la umbali wa mita 35 kuzama moja kwa moja upande wa juu kulia wa goli la Mauritania na kufanya filimbi ya mwisho matokeo kuwa 3-2. Chanzo: mwananspoti
 TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)

No comments:

Post a Comment