MAELFU ya wakazi wa mkoa wa Iringa
na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na Serikali
wakiongozwa na Rais Dr Jakaya Kikwete wameshiriki katika mazishi
ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga na waziri wa fedha Dr
Wiliam Mgimwa.
Huku
waziri mkuu Mizengo pinda katika salam zake za serikali akielezea
jinsi ambavyo Taifa lilivyopata pigo kubwa kufuatia kifo cha Dr
Mgimwa kutokana na mchango wake katika baraza la mawaziri.
Katika mazishi hayo yaliyofanyika
leo kijiji kwake Magunga jimbo la Kalenga wananchi mbali mbali
walionyesha kujipanga barabarani kutoka Manispaa ya Iringa hadi
kijijini kwake huku wakiupungia mkono msafara wa rais Kikwete na
baadhi yao wakilazimika kutumia usafiri wa baiskeli na pikipiki
kwenda katika mazishi hayo.
Akitoa shukrani za familia kwa niaba
ya familia mtoto wa marehemu Dr Mgimwa Godfrey Mgimwa aliishukuru
serikali kwa jinsi ambavyo ilivyohangaika kumuuguza baba yake na
kutoa wosia mzito wa marehemu Dr Mgimwa ambao alimtaka kuufikisha
kwa Rais Kikwete..
Alisema
katika uhai wake kabla ya kifo chake ikiwa ni siku tano kabla Dr
Mgimwa alimwita na kumtaka kufikisha shukrani zake kwa Rais
Kikwete kwa kumtembelea mara mbili Hospital alipokuwa amelazwa
pamoja na spika wa bunge Anne makinda .
Pia alisema kuwa alieleza dhamira
yake ya kuwatumikia wana Kalenga na kusema zawadi kubwa ni msaada
wa bati zaidi ya 2000 kwa wananchi hao ili kuendeleza ujenzi wa shule
na vituo vya afya jimboni.
"Baba kabla ya kufa aliniachia wosia
huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru kwa ushirikiano wao na
kutoa bati ila alipenda kuona Kalenga inakuwa na maendeleo zaidi"
Kwa upande wake waziri Mkuu Pinda
alisema kuwa serikali imepata pigo kubwa juu ya kifo hicho na kuwa
bado serikali itaendelea kuwa karibu na familia ya Dr Mgimwa na pale
penye tatizo isisite kuwasiliana .
Hata hivyo Rais Kikwete hakupata
kuzungumza chochote katika msiba huo zaidi ya kuweka mchanga na
shada la maua pamoja na kuwapa mkono ndugu wa Dr Mgimwa .
Spika wa bunge Anne Makinda alisema
kuwa bunge limempoteza kiongozi na mbunge aliyependa kutumia nafasi
yake kwa ajili ya Taifa na kuwa kamwe mchango wake hawataacha
kuukumbuka.PICHA NA HABARI KWA HISANI YA FRANSIS GODWIN IRINGA
|
No comments:
Post a Comment