Mkwasa (mwenye rangi za Bluu) akiongoza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Bora Mabatini Kjitonyama
Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu ya Young Africans
leo imeeanza kujifua katika viwanja vya bora Mabatini Kijitonyama
kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa
chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.
Young
Africans ilisimama kufanya mazoezi kwa siku takribani tatu kufuatia
kufanya mabadiliko ya benchi la Ufundi na leo rasmi imeanza mazoezi
asubuhi chini ya makocha wasaidzi Mkwasa na kocha wa makipa Juma
Pondamali.
Mkwasa
alitumia muda wa dakika 5 kuongea na wachezaji wote waliofika mazoezini
siku ya leo, kuwaelekeza nini wanapaswa kufanya na kuzingatia mafunzo
yake ambapo wachezaji waliweze kutekeleza kwa kiwango cha hali ya juu.
Kocha
wa makipa Juma Pondamali aliwafua vilivyo magolikipa Juma Kaseja, Ally
Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida" na kusema huu ni mwanzo tu
kwani anaamini wachezaji hao watakua katika kiwango kizuri kutokana na
uwezo wanaouonyesha katika mazoezi anayaowapatia.
Kikosi
cha Young Africans kesho kitaendelea na mazoezi asubuhi katika uwanja
wa Mabatini Kijitonyama ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa
pili na mashindano ya kimataifa.
Aidha
washambuliaji Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi waliokwenda kwao nchini
Uganda kwa ajili ya matatizo ya kifamilia wanatarajiwa kurejea nchini
mwishoni mwa wiki tayari kuungana na wenzao kujiandaa na mzunguko wa
pili.
No comments:
Post a Comment