Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa
Maofisa wa Jeshi la Magereza (hawapo pichani) katika sherehe za kuaga
Mwaka 2013 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014. Sherehe hizo zimefanyika
jana katika Viwanja vya Bustani ya Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga,
Jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza mmoja wa
Maofisa wa Jeshi la Magereza, Stafu Sajin Luckson Mtenga ambaye
amezawadiwa zawadi ya Kipoza Joto kutokana na kutenda kazi zake kwa
kujituma na kuonesha nidhamu kiutendaji kwa Mwaka uliopita wa 2013.
Makamanda
na Wapiganaji wa Jeshi la Magereza wakipata vinywaji vya aina
mbalimbali katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.
Maofisa
na Askari wa Jeshi la Magereza wakipita mbele ya Mgeni rasmi kwa ajili
ya kutosi glasi za vinywaji katika Sherehe ya kuukaribisha Mwaka mpya wa
2014.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Magereza(waliosimama) ambapo
wamezawadiwa zawadi ya Kipoza Joto(Refregerator) kila mmoja kutokana na
kutenda kazi zao kwa kujituma kwa Mwaka uliopita 2014(wa pili kulia) ni
Mke wa Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Frola Minja(wa pili kushoto)
ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa kwanza
kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa( wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston
Sanga.
No comments:
Post a Comment