Mahakama
ni Chombo cha kutoa haki. Nimeomba mahakama kuzuia kamati kuu ya chama
changu kunijadili mpaka rufaa yangu isikilizwe na Baraza Kuu la chama.
Sijaomba kuzuia kamati kuu kuendelea na kikao chake. Nimeomba kamati
isinijadili maana nina rufaa kwenda Baraza Kuu kwa jambo hilo hilo
ambalo kamati kuu inataka kuliamulia. Wakili wa chama Tundu lissu
aliweka mapingamizi akisema mahakama haina mamlaka kujadili masuala ya
vyama na wanachama wao. Jaji John Utumwa katupilia mbali mapingamizi
yote yaliyowekwa na Tundu Lissu.
Mahakama ndio Chombo cha kutoa haki. Asante Wakili Albert Msando.
Haki itatendeka tu.- Zitto Kabwe
No comments:
Post a Comment