Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 5, 2014

SIMBA WAFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI,WAICHAPA KMKM GOLI 1 BILA

 
PICHA NA BINZUBERY

Pambano limemalizika Simba wameshinda goli lile lile moja lililopachikwa na Amri Kiemba dakika ya 4 kutokana na mpira wa pembeni kulia uliopigwa na William Lucian na mfungaji akaukwamisha kimiani kwa kichwa huku walinzi watatu na mlinda lango wa KMKM Mudathir Khamis wasijue la kufanya.

TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Ni pambano lililokuwa na kasi ya aina yake kwa dakika zote tisini huku KMKM wakifanya kila njia kusawazisha bila mafanikio.

Dakika kumi na tato za mwisho wenyeji waliliandama lango la Simba na mara mbili wakimlazimisha kipa Yaw Berko kufanya kazi ya ziada kuokoa mipira iliyokuwa ikielekea langoni na kuwa kona ambazo hata hivyo hazikuzaa matunda.

Mbali na goli la Kiemba ambalo lilikuwa la kiufundi, tukio lingine kubwa katika mchezo huo ilikuwa ni kocha wa KMKM, Ally Bushiri kkuamuriwa na mwamuzi Waziri Sheha kuondoka kwenye benchi na kujumuika na mashabiki jukwaani kufuatia kudaiwa kutoa lugha chafu kwa mwamuzi huyo anayetambuliwa na Shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu, FIFA.

Kwa matokeo hayo sasa kundi B limekuwa la kwanza kukamilisha michezo yake huku KCC ya Uganda ikiongoza kwa kukusanya pointi 7 sawa na Simba lakini waganda hao wana tofouti kubwa ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Timu mbili za juu kwa katika makundi matatu zinafunzu moja kwa moja kwa robo fainali wakati timu mbili zitatoka miongoni mwa timu tatu zitakazomaliza katika nafasi ya tatu ili kukamilisha timu nane za robo fainali.

Kundi la A lililoko Pemba litamaliza michezo yake Jumatatu kwa Mbeya City kuwakabili waganda URA huku Chuoni wakipambana na ndugu zao Cloves Stars.

Kwa upande wa Unguja Azam wenye pointi sita watacheza na Ashanti United saa mbili usiku baada ya mchezo wa mapema saa 10 join kati ya Tusker ya Kenya na Spice Stars.

Ahasante kwa kuungana nasi siku ya leo tutakuwa wote tena kesho.MAELEZO NA AZAM TV

No comments:

Post a Comment