Pages

Friday, January 24, 2014

TAARIFA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA NCHINI LEO


Gazeti la Tanzania Daima la tarehe 23 Januari, 2013 liliandika makala inayosomeka "JK AMNUSURU MFUNGWA WA EPA". Gazeti hilo lilidai mfungwa wa kesi ya EPA Ajay Somani ametolewa gerezani kwa njia ya kutatanisha wakati wafungwa wengine waliokuwa kesi moja wanaendelea kusota gerezani.
Maelezo mafupi kuhusu suala hilo ni kwamba mfungwa Na. 74/2012 Ajay Suryakant Somani tarehe 22 Novemba, 2012 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu shauri la Jinai Na. 1164/2008 kwa kosa la "Obtaining Money by False Pretence c/s 302 of the Penal Code".

Watuhumiwa wenzake katika kesi hiyo walikuwa Sophia Joseph Lalika, Ester Komu na Emmanuel Mwakyosa. Hawa walikuwa wanakabiliwa na shtaka la "Occasioning Loss to a Specified Authority". Hawa walihukumiwa
kifungo cha miaka mitatu au faini shilling! milioni tano (Tzs.5,000,000/=) kila mmoja. Wafungwa wawili Ester Komu na Emmanuel Mwakyosa walilipa faini siku hiyo hiyo mahakamani na kuachiliwa huru. Mfungwa Sophia Joseph Lalika kwa kuwa hakulipa
faini hiyo mahakamani alipelekwa gerezani na tarehe 23/11/2012 alilipa faini hiyo na kuachiliwa huru. Hivyo madai yaliyotolewa kwamba bado wanasota gerezani siyo ya kweli.
Kuhusu Mfungwa Na. 74/2012 Ajay Suryakant Somani wakati akiendelea na kifungo chake gerezani alipata mapunguzo ya 1/6 ya kifungo chake kwa msamaha wa Rais uliotolewa kwa wafungwa tarehe 9 Desemba, 2013 wakati wa kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa nchi yetu. Mapunguzo haya ya 1/6 ni zaidi ya mapunguzo ya kawaida 1/3 yanayotolewa chini ya Sheria ya Magereza ya mwaka 1967. Kutokana na msamaha huo kifungo chake kupunguzwa kwa nusu (1/3 + 1/6 = 1/2) yaani mwaka mmoja na kwa hali hiyo kustahili kuachiliwa huru tarehe 9/12/2013.
Wafungwa wengine waliotajwa No.247/2011 Farijala Shabani anayetumikia kifungo cha miaka kumi na moja (11) na Na. 345/2011 Rajabu Maranda anayetumikia kifungo cha miaka kumi (10) nao walinufaika na msamaha huo wa Mhe. Rais lakini waliendelea kubaki gerezani kutokana na urefu wa vifungo vyao.

Hivyo Gazeti husika lifute kauli hiyo kwa kuwa waliachiliwa huru kwa
mujibu wa sheria na kwa sasa ni raia huru.

John C. Minja 
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
23 Januari, 2014

No comments:

Post a Comment