John Mnyika-Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema |
Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya
habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho, Chama kimetoa kauli
ifuatayo;
Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho tarehe 3
Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni
tatu;
Mosi: Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba
Kamati Kuu itapokea taarifa juu yakupitishwa kwa marekebisho ya sheria
ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa
2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya
Katiba Mpya.
Pili: Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao.
Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha
utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa
ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya
kikao kinachohusika.
Tatu: Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014
Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati
wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati
makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.
John Mnyika
Mkurugenzi wa Mawasiliano
No comments:
Post a Comment